In Summary

• Alisema kwa sasa anatafuta mfanyabiashara makini ambaye atamuingizia pesa za kusaidia wazo lake kuanza.

• Alisema hataki kuteseka kimya kimya na hivyo kuamua kutafuta usaidizi kutoka kwa Wakenya.

Kimani Mbugua
Image: HISANI

Aliyekuwa Mwanahabari wa Citizen TV Kimani Mbugua ametoa wito kwa Wakenya kumsaidia kurejesha maisha yake baada ya kutoka hospitalini.

Katika video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii siku ya Jumapili, Mbugua alisema aliugua mwaka wa 2020 na aligunduliwa na ugonjwa wa bipolar wa hisia za kubadilika-badilika.

“Nilitoka hospitalini wiki iliyopita na nahisi akili yangu imerejea katika hali ya kawaida na sitaki kurejea mahali nilipokuwa zamani,” alisema.

Mbugua alibainisha kuwa kwa sasa hana makao kwani watu waliomkaribisha hapo awali walimwambia atafute mahali pengine pa kuishi.

"Nilikuja kutafuta mtu mwingine ambaye angeweza kunikaribisha lakini sikumpata. Ninahitaji tu msaada wako," alisema.

Mbugua alisema kwa muda wa wiki moja ametoka hospitalini, tayari amekuja na mpango wa biashara na pendekezo lake la kwanza kwa mteja mwenye muundo wa kampuni.

Alisema kwa sasa anatafuta mfanyabiashara makini ambaye atamuingizia pesa za kusaidia wazo lake kuanza.

Alisema hataki kuteseka kimya kimya na hivyo kuamua kutafuta usaidizi kutoka kwa Wakenya.

"Niligundua kuwa naweza kuteseka kimya kimya na nisiseme na kushuka moyo tena na kurudi kwenye dawa za kulevya. Sitaki kurejea kwenye dawa za kulevya," alisema.

Mbugua alisema hajatumia dawa kwa muda wa miezi miwili na hatataka kurejea tena. Alisema alikuwa akitumia vibaya bangi na sigara.

Alisema hatimaye yuko katika hatua ya kupona hata kama hana paa juu ya kichwa chake.

Alisema alipoteza sana ikiwa ni pamoja na marafiki katika safari yake ya kupona.

“Niko katika hali ambayo watu wengi hawako tayari kusaidia, wanasema wamechoka,” alisema.

Alibainisha kuwa hata aliazima simu ambayo aliitumia kuchukua video hiyo akiomba msaada na kuiweka kwenye mitandao ya kijamii.

“Ukitaka kunisaidia, barua pepe yangu ni danielkimani2027@gmail.com,” alisema.

Kimani aliingia katika tasnia ya habari akiwa na umri wa miaka 19 alipojiunga na Nation Media Group kama mwanafunzi wa chuo kikuu katika mafunzo.

Alifanya kazi na idara ya redio katika Nation kwa miaka mitatu kabla ya kujiunga na Royal Media Services ambako alifanyia kazi Citizen TV, Inooro fm na Hot 96.

View Comments