In Summary

• Pia alitumia fursa hiyo kama kaka mkubwa kuwapa ushauri watoto hao kwamba wakati wanaendelea kung’ang’ana na masomo, wasimuache wala kumsahau Mungu.

Harmonize
Image: Insta

Usiku wa Jumamosi Harmonize alitia joto kwenye nyoyo za watoto takribani 20 hivi baada ya kuwapa nafasi adimu ya kujiunga naye kwenye studio zake za Konde Gang kurekodi ngoma nao.

Msanii huyo alipakia klipu hizo akiwa na watoto hao kwenye studio wakirekodi kile kilichoonekana kama ni wimbo wa injili wakiimba ‘hallelujah’.

Harmonize kwenye video ya kwanza aliandika kwamba ilikuwa ni nafasi ya kufarijika sana kujumuika na watoto hao ili kuwapa nafasi ya kupaisha vipaji vyao kwatika uimbaji.

“Usiku wa Baraka ulioje ameen, hatimaye nilibahatika kurekodi wimbo ambao nimekuwa nikiota kuufanya. Niko na uhakika hawa [watoto] watakaokuwepo  kwenye kuvipa Amani vizazi na vizazi,” Harmonize aliandika akionesha jinsi amekuwa na uchu wa kufanya wimbo wa sampuli hiyo kwa muda sasa.

Harmonize aliwataja watoto hao kama malaika na kusema kuwa alishawapa ahadi kwamba yeyote atakayefaulu katika changamoto hiyo ya kurekodi basi ako radhi kufadhili masomo yake hadi ngazi za mwisho kabisa chuo kikuu.

“Niliwaambia malaika hawa yeyote atakayefaulu kwenda shule ya sekondari, gharama zote zitakwua chini yangu hadi afike chuo Ishaalah, ameeni. Nina furaha kwamba tuliweza kufanya hili pamoja, Mungu awabariki sana,” Harmonize alitoa ahadi hiyo.

Pia alitumia fursa hiyo kama kaka mkubwa kuwapa ushauri watoto hao kwamba wakati wanaendelea kung’ang’ana na masomo, wasimuache wala kumsahau Mungu.

“Someni sana, msimuache Mungu wadogo zangu, nipo hapa kwa ajili yenu,” alishauri.

 

View Comments