In Summary

• Baada ya kuachana, Goergina alikwenda mitandaoni akipakia msururu wa picha akiwa na tattooe mfanano na jamaa ambaye hakuweza kumuonesha sura yake.

Gerogina Njenga
Image: Insta

Aliyekuwa mpenzi wa muigizaji Tyler Mbaya maarufu kama Baha Machachari, Georgina Njenga amejitetea kwamba kama si tafrija za wikendi, angekuwa mke mzuri sana wa kuolewa na kuwekwa ndani.

Mama huyo wa mtoto mmoja alifichua haya kupitia Insta story yake ambapo alipakia video akiwa kwenye bwawa la kuogelea akiwa ameshika bilauri yenye kinywaji mkononi na kuandika;

“Mimi ni wife material, shida ni Ijumaa, Jumamosi na Jumapili.”

Njenga ambaye yuko singo alifichua miezi michache iliyopita kwamba yeye na baba mwanawe, Tyler Mbaya si wapenzi tena lakini akakiri kwamba kijana huyo ni baba mzuri anayempenda binti yao, Astra na kwamba anamsaidia katika malezi.

Baada ya kuachana, Goergina alikwenda mitandaoni akipakia msururu wa picha akiwa na tattooe mfanano na jamaa ambaye hakuweza kumuonesha sura yake.

Alipokuwa anawajibu mashabiki wake kwenye kipindi cha maswali na majibu Instagram, aliulizwa ikiwa yeye na Baha ni wapenzi lakini akakataa na kusema kwamba umepita muda mrefu tangu walipoachana.

Pindi baada ya kufichua hilo, wikendi iliyofuata Georgina alionekana kwenye klabu akimega sherehe huku akibugia shisha.

Bila shaka hilo linathibitisha kauli hiyo yake kwamba pasingekuwa na sherehe za wikendi kama hizo ambazo anazifagilia sana, angekuwa mke mzuri sana wa kuolewa.

Tangu kuachana na Baha, muigizaji huyo hajawai onekana hadharani akizungumzia kilichokwamisha uhusiano wao lakini Georgina akifanya mahojiano na Mungai Eve alisema kwamba kuachana kwao kulikuja si kutokana na kashfa ya utapeli ya Baha bali ni maelewano ya pande zote baada ya kile alisema ni “Kuchoka na mapenzi kuisha”.

View Comments