In Summary

• Kwenye mazungumzo ya moja kwa moja na Clouds Fm Aslay ametangaza ujio wa Tamasha la kusherehekea miaka kumi ya makubwa yake kwenye muziki.

ASLAY/INSTAGRAM

Msanii wa nyimbo za Bongo Aslay, jina lake kamili Aslay Isihaka Nassoro, Amewaalika mashabiki wake katika tamasha la kuadhimisha miaka kumi kwenye tasnia ya muziki.

Kwenye mazungumzo ya moja kwa moja na Clouds Fm Aslay ametangaza ujio wa Tamasha la kusherehekea miaka kumi ya mafanikio yake kwenye muziki.

Amesema kwamba ataburudisha nyimbo 100 mbele ya mashabiki wake mnamo Septemba 30 usiku katika ukumbi wa Warehouse Masaki Dar es salaam kama njia moja ya kuadhimisha siku hiyo.

"Miaka kumi ya Aslay katika Game,kuna vitu mingi nimepitia ndani ya game, kwa hiyo ni muda sasa wa kutioa shukrani zangu kwa zambiki zangu na kuwaonyesha kwamba Aslay bado yuko kwenye game."

Amewapongeza mashabiki wake ambao kulingana na yeye wamechangia pakubwa katika safari yake ya kukua kimuziki.

"Natoa shukrani zangu kwenye mashabiki ambao wamesimama na mimi kwenye mabaya na katika mazuri na kuwaonyesha kwamba bado nipo na natoa burudaki kama kawaida."

Alienda mbele kusema kwamba aijalishi kwamba hapo katikati amekuwa kimya ila amepata management mpya ambayo anapanga makubwa nao.

Ameongeza kwamba ni nafasi ambayo alikua aniomba sana kwa Mungu ili kupata nafasi kama hii ya kushukuru kwa yale yote amepitia tangu alipoanza muziki.

Aidha amesema kwamba amealika wasanii wengi ambao watajiunga naye katika tamasha hiyo kubwa ya miaka kumi ya Aslay kwenye muziki.

Wasanii wengine mashuhuri amesita kuwataja akisema ni kama surprise kwa mashabiki.

View Comments