In Summary

•Tangu wakati wa covid amepata wafuasi zaidi ya milioni 160 kwenye TikTok yake na kufuatiliwa na milioni 2.4.

Mwana Tiktoker Khaby Lames

Mkali wa TikTok Khaby Lame ambaye amekuwa akiwaburudisha wafuasi wake bila kuzungumza neno lolote ametajwa kuwa mtayarishaji mashuhuri wa jarida la Forbes.

Jarida hili lilikadiria mapato ya Lame kuwa 16.5 milioni (Sh2.4 bilioni) kufikia Juni 2022,Hii ilitokana na uidhinishaji ambao mshawishi huyo amekuwa nao tangu mafanikio yake.

Lame aliambia  jarida la Forbes kuwa kwa kila chapisho analochapisha kwenye TikTok na Instagram, anapata jumla ya millioni (Sh110,000,000).

Forbes waliripoti kuwa Lame amefanya kazi na Kampuni kama vile; Hugo Boss, Binance na benki  QNB.

Mwana tiktoker huyo mwenye umri wa miaka 23 pia aliiambia Forbes kwamba kampuni  anazofanya nazo kazi lazima zipate mwelekeo kutoka kwa familia yake na marafiki, hili zisijumuishi pombe, sigara na bidhaa yoyote mbaya kwa matumizi ya binadamu.

“Ninakataa maombi mengi,Nataka kufanya kazi safi, Sijawahi kufanya kazi na kampuni ya pombe, sigara au kitu chochote ambacho ni mbaya kwa sababu watoto wengi hunifuata," alisema.

Mshawishi  huyu wa Italia alikua maarufu zaidi wakati wa janga la Covid-19.

Tangu wakati huo amepata wafuasi zaidi ya milioni 160 kwenye TikTok yake na kufuatiliwa na milioni 2.4.

“Nilipoanza kutengeneza video, watu waliniambia nipate kazi inayofaa,Lakini niliendelea kutengeneza video kwa sababu ndivyo ninapenda kufanya, ingawa hakuna mtu aliyekuwa akizitazama,” aliiambia Forbes.

Ili kuorodhesha Lame kama mtayarishi mashuhuri zaidi, Forbes ilisema ilitumia data kuhusu mapato, hesabu za wafuasi, viwango vya ushiriki na shughuli za ujasiriamali za maelfu ya watu mashuhuri kwenye mtandao kwa usaidizi wa kampuni ya wabunifu ya uuzaji.

View Comments