Mama Dangote afunguka, atamani Diamond aoe lakini hajafanikiwa
Msanii Diamond kwa sasa hajafanikiwa kuwa na ubavu wake wa kudumu
•Natamani mwanangu Diamond aoe hata kama ni sasa hivi ila lakini huenda yeye hajafanikiwa kupata ama labda mwenyezi mungu hajampa ubavu wake ila kila siku namwambia mwanangu Naseeb oa mpaka wakati mwingine nawatuma marafiki na dada zake waongee naye
Furaha ya Mzazi ni kuona wanae wakifanikiwa kwa kila jambo wafanyao kwa maisha ila kwa sasa Mama Dangote amejawa na kiu ya kuona mwanae Diamond akifanikiwa kwa Ndoa
Licha ya kuwa nyota wa muda mrefu wa nyimbo za Bongo msanii Diamond kwa sasa hajafanikiwa kuwa na ubavu wake wa kudumu baada ya kusabaratika kwa mahusiaono ya mapenzi dhidi ya Zari Hassan,Wema sepetu ,Tanasha Donnah na wengine ambao walichumbiana kwa muda.
Jambo ambalo linamtatiza Mama Dangote ambaye ni mamake mzazi aliyefunguka jambo hili kwenye mahojiano ya moja kwa moja na kituo cha Radio Wasafi FM .
"Natamani mwanangu Diamond aoe hata kama ni sasa hivi ila lakini huenda yeye hajafanikiwa kupata ama labda mwenyezi mungu hajampa ubavu wake ila kila siku namwambia mwanangu Naseeb oa mpaka wakati mwingine nawatuma marafiki na dada zake waongee naye ."alisema .
Diamond kwa sasa kwenye mitandao duru zinaarifu kuwa huenda wanachumbiana na Zuchu ambaye ni mmoja wa wasanii waliosajiliwa chini ya mwavuli Wasafi Records WCB.
Ila mapenzi haya kulingana wabebesi yanakubwa na matatizo kwa kile wanachodai Diamond kuwa karibu sana na mtoto wa aliyekuwa mpenzi wake Tanasha Donnah