In Summary

•Katika video aliyoshirikishwa kwenye chaneli yake ya YouTube, mwimbaji huyo alifichua kuwa hajawahi kutangaza habari hiyo hadharani

•Wengi wenu mnajua kuwa nina watoto watatu, Nathaniel, Malaki ambaye yuko mbinguni, na Natalie pamoja nami. Lakini ukweli ni kwamba nina watoto wanne.

Kambua/Instagram

Mwimbaji wa nyimbo za injili Kambua amefunguka kuhusu malezi na kufichua kumpoteza mtoto mwingine.

Katika video aliyoshirikishwa kwenye chaneli yake ya YouTube, mwimbaji huyo alifichua kuwa hajawahi kutangaza habari hiyo hadharani.

"Wengi wenu mnajua kuwa nina watoto watatu, Nathaniel, Malaki ambaye yuko mbinguni, na Natalie. Lakini ukweli ni kwamba nina watoto wanne. Hiki ni kitu ambacho sijawahi eleza umma, lakini nadhani ni wakati wa kukuleta katika ulimwengu wangu na kukuambia juu ya watoto wawili ambao waliaga na wawili ambao nalea," alisema.

Kambua hakufichua ni lini hasa alimpoteza mtoto wake mwingine kwani sehemu ya kwanza ya hadithi iliangazia zaidi uhusiano wake na baba yake najinsi alivyokutana na mumewe.

Mnamo Februari 2021, mwimbaji huyo wa nyimbo za injili alitangaza kuwa amempoteza mwanawe , Malachi. 

 Kambua alitangaza habari hiyo ya kuhuzunisha katika ujumbe wa hisia kwenye ukurasa wake wa Instagram.

"Malachi is now free from pain and any worldy care. Our tears fall freely because our hearts are broken beyond words. But our faith and hope remain unshaken because we have our trust in a dependable God. You were deeply loved and will forever be remembered. Your father, your mommy, and your brother Nathaniel, will carry you in our hearts always," she wrote," Kabua aliandika.

Kambua, alichapisha video  inayosimulia safari yake.

 

View Comments