In Summary

•Kwenye mazungumzo,Dem wa Fb alisema kwa ujasiri kwamba yeye bado ni bikira.

•`Wacha tu nipigwe na baridi kwa sababu  mimi ni bikira,bado sijaguswa,tangu nizaliwe sijawahi kupatana na mwanaume kimapenzi.``

Dem wa Fb

Muunda maudhui maarufu anayejulikana kwa majina la utani kama Kienyeji Finest,almaarufu Demu Wa Fb, amesema bado yeye ni bikira.

Kwenye mazungumzo,Dem wa Fb alisema kwa ujasiri kwamba yeye bado hajaguswa na chuma, ni bikira.

``Wacha tu nipigwe na baridi kwa sababu  mimi ni bikira,bado sijaguzwa,tangu nizaliwe sijawahi kupatana na mwanaume kimapenzi.``

Mcheshi huyo aliendelea kujieleza akisema kwamba anatosheka na umbo lake ambalo anajivunia kupewa na Mungu akisema hana haja ya kujipaka vipodozi.

Alisema kwamba kwa jinsi anavyojiamini ,anahofia kutumia vipodozi kwani huenda akavunja ndoa za watu, akieleza  jinsi wanaume watakavyo mtamani.

Sina haja ya kutumia vipodozi kwa sababu sitaki kuvunja ndoa za watu,najua nikianza kutumia vipodozi nitawachanganya wengi.

Mcheshi huyo amewahujumu wanadada ambao wanatumia virembesho,ambazo kwa madai yake vinaleta matatizo kwa ndoa ,kwa kubadilisha muonekano wakiwa  bila vipodozi. Jambo ambalo amesema linachangia udanganyifu wa kimapenzi katika ndoa.

Kama mtayarishaji wa maudhui, Dem Wa Facebook anajulikana kwa uwepo wake mzuri wa jukwaa na uwezo wa kushirikisha watazamaji.

Mara nyingi alichaguliwa kama MC wa hafla za shule, akiburudisha kwa  maonyesho yake ya kuvutia.

 

 

View Comments