In Summary

• Ezekiel alisema kwamba ukiona mwanamke ambaye amevalia earrings Zaidi ya tatu masikioni mwake, jua moja kwa moja kwamba huyo anaandamwa na nyota ya talaka.

mchungaji Ezekiel Odero
Image: Facebook

Mchungaji mwenye utata, Ezekiel Odero amezua minong’ono mitandaoni baada ya kudai kwamba anajua maelezo ya mavazi ya mwanamke ambaye ni changudoa.

Katika mahubiri kanisani mwake na ambayo video yake imeenezwa mitandaoni, mchungaji huyo anayejitapa kuwa na uwezo wa kurudisha nyota ya ndoa alidai kwamba mwanamke anayevaa mapambo ya masikioni maarufu kwa kimombo kama earrings ni sawa na kujitafutia matatizo katika ndoa yake.

Ezekiel alisema kwamba ukiona mwanamke ambaye amevalia earrings Zaidi ya tatu masikioni mwake, jua moja kwa moja kwamba huyo anaandamwa na nyota ya talaka.

“Kuna mtu anaitwa Ezekiel, Mungu amempa neema ya kurudisha watu waliopewa talaka, wewe ulipewa talaka moja, kuna mwingine alipewa tatu, unataka bwanako?” Ezekiel alimuuliza mwanamke mmoja aliyekwenda katika kanisa lake akiwa na vyeti vya ndoa na talaka.

Kabla ya kumjibu swali lake, Ezekiel aligundua kwamba mwanamke huyo alikuwa na earrings tatu kwenye sikio lake.

“Hizi huwa ni certificates za talaka,” Ezekiel alisema huku akirejelea earrings kwenye sikio la mwanamke huyo. “Ukiziweka hivi, ni makahaba ndio wanaziweka nyingi. Lakini ile roho ya talaka ndio inakuambia vaa hizi, mbili hazitoshi, vaa tatu. Roho ya talaka inakuambia vaa nguo, wacha kifua wazi watu waone, vaa nguo miguu yako ionekane, kwa nini unafunika miguu,” Ezekiel alisema.

Mchungaji huyo alisisitiza kwamba roho ndio humuambia mtu kitu na uamuzi wa kufanya.

 

 

View Comments