In Summary

• “Ama ningewekeza katika kitu kingine kweney uwekezaji wangu, chenye dhamani, ila niliamini katika furaha yangu" Harmonize.

Image: INSTAGRAM// HARMONIZE

Msanii Harmonize anazidi kujuta kumwaga pesa nyingi kwa ajili ya kujaribu kustawisha penzi lake na Kajala am balo hata hivyo lilibuma.

Sanii huyo ambaye amekuwa akionesha dalili za kujuta tangu walipoachana na Kajala kimya kimya mwishoni mwa mwaka jana, aliandika aya ndefu kupitia Instagram story yake akisema kwamba bado hajatosheka kumwaga mtama kuhusu kile kilichokuwa kikiendelea wakati wa uhusiano wake wa unyonyaji na Kajala.

Harmonize aliahidi kwamba hivi karibuni ataendelea kufanya ufichuzi, akisema kwamba kuna baadhi ya matukio ambayo mashabiki wake wanajua ya mengine wasiyoyajua.

“Kuzungumzia kuhusu mapenzi, nimepitia visa na mikasa mingi sana ya kimapenzi 2023, mnavyovifahamu na msivyo. Muda na pesa nilizowekeza kwenye mahusiano ningalikuwa nampe mwanamke wa Tanzania bila shaka tungeshakuwa na mwanadada mjasiriamali bora mtanzania,” sehemu ya ujumbe huo wa kujuta ulisoma.

Harmonize alizidi kuteta kwamba laiti angewekeza hela alizomhonga Kajala nazo pengine sasa hivi angalikuwa anatazamia matunda mema.

“Ama ningewekeza katika kitu kingine kweney uwekezaji wangu, chenye dhamani, ila niliamini katika furaha yangu maana siku zote my peace of mind comes first. Napenda kuwa mwenye furaha niendelee kuwahudumia [mashabiki wangu] kwa muziki bora pia nipate muda wa kutengeneza afya bora na ndio maana chochote kinachohusisha Amani ya moyo wangu nakipa asilimia kubwa,” Harmonize aliendelea kujuta.

Msanii huyo alitoa hayo kama kidokezo tu cha yale ambayo yanaendelea kumbemenda ndani kwa ndani lakini akasema kwamba Oktoba 14 atakuwa na tamasha lake Dar es Salaam ambapo aliahidi kuzungumza machache na mashabiki wake kupitia kwa waandishi wa habari za mitandaoni.

View Comments