In Summary

• Mwezi uliopita, alilazwa katika hospitali moja nchini Marekani kwa masuala hayohayo, jambo lililomfanya babake amsihi aache pombe kwa ajili ya maisha yake marefu.

• Daniella na Chameleone, licha ya kutengana, wanaendelea kugawana watoto sita.

Mkewe Chameleone amruka katika sakata la kumpiga mtu nyaunyo
Image: Instagram

Kwa muda mrefu kumekuwa na uvumi kuhusu kutengana kwa msanii wa muda mrefu wa Uganda, Jose Chameleone na mkewe, Daniella, huku fununu zikipendekeza unyanyasaji wa nyumbani ndio chanzo.

Iliaminika kuwa Daniella alilazimika kutoroka nchini na watoto wao kutokana na kushambuliwa mara kwa mara na Chameleone. Sasa amekuwa akiishi Marekani kwa zaidi ya miaka mitatu.

Hata hivyo, katika mahojiano ya hivi majuzi na MwanaYouTube, hatimaye Daniella alifunguka kuhusu sababu halisi ya kutengana kwao - uraibu wa pombe wa Chameleone.

"Chameleone alikuwa anakunywa pombe kupita kiasi, mara nyingi akirudi nyumbani saa tisa au saa kumi alfajiri au hata saa kumi na moja alfajiri, hawezi kujihudumia mwenyewe. Siku zote alikuwa amelewa. Nilieleza wasiwasi wangu na kumsihi abadilishe tabia yake, hasa kwa sababu tulikuwa tumekua."

“Sikutaka awe mfano mbaya kwa watoto wetu. Kwa bahati mbaya, alikataa kubadilika. Siku moja, nilimpa amri ya kuchagua kati yangu, watoto wetu au pombe, alichagua pombe. Hapo ndipo nilipolazimika kufanya uamuzi mgumu kuondoka," alieleza mkewe Chameleone.

Unywaji pombe kupita kiasi wa Chameleone uliathiri afya yake, hivyo kupelekea kuzuru hospitali mara nyingi kutokana na matatizo ya tumbo na ini, yote yakichangiwa na unywaji wake wa pombe.

Mwezi uliopita, alilazwa katika hospitali moja nchini Marekani kwa masuala hayohayo, jambo lililomfanya babake amsihi aache pombe kwa ajili ya maisha yake marefu.

Daniella na Chameleone, licha ya kutengana, wanaendelea kugawana watoto sita.

View Comments