"Nitakumis"-Milly Wa Jesus ashikwa na hisia wakati akimuaga mumewe
Wapenzi hao walikumbatiana kwa uchangamfu huku wakipeana mabusu,walijaribu kuzuia machozi yao walipoonana kimwili kwa mara ya mwisho kabla ya Kabi kuondoka.
•Milly alibainisha kuwa ilikuwa ni mara ya kwanza katika miaka sita ya ndoa yao kwamba wanandoa hao watakuwa mbali kwa muda mrefu.
•"Nina hisia kali sana. Nimekuwa nikilia. Sitaki Kabi anione nalia kwa sababu sitaki apate hisia. Tumezoea kufanya kila kitu pamoja, najua watu wengine wanaweza kusema huenda nimekasirika, lakini kufikiria kuwa hayupo kwa muda mrefu ni ngumu sana, "
Muunda maudhui Milly Wa Jesus alishikwa na hisia na kudondokwa na machozi wakati mume wake mpendwa, Kabi, akiondoka kuelekea Uchina.
Milly alibainisha kuwa ilikuwa ni mara ya kwanza katika miaka sita kwenye ndoa, kwamba wawili hao watakuwa mbali kwa muda mrefu.
Mwanablogu huyo alisema kuwa angesongwa na mawazo kwa muda wote ambao atakuwa mbali na mumewe jambo ambalo si la kawaida kwake.
Katika video aliyoshiriki kwenye ukurasa wake wa YouTube, Milly alijaribu kuzuia machozi yake wakati akitoa hisia ambazo atakumbana nazo za upweke bila mumewe.
"Nina hisia kali sana. Nimekuwa nikilia. Sitaki Kabi anione nalia kwa sababu sitaki apate hisia. Tumezoea kufanya kila kitu pamoja, najua watu wengine wanaweza kusema huenda nimekasirika, lakini kufikiria kuwa hayupo kwa muda mrefu ni ngumu sana, "alisema kwa machozi.
Milly na Kabi walishiriki wakati wa kimahaba katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) wakati wa kuagana.
Wapenzi hao walikumbatiana kwa uchangamfu huku wakipeana mabusu. Wote wawili walijaribu kuzuia machozi yao walipoonana kimwili kwa mara ya mwisho kabla ya Kabi kupanda ndege yake kuelekea Uchina.
Baadhi ya mashabiki wanaomfuatilia kwenye mitandao walielekea kwenye sehemu ya maoni ili kushiriki maoni yao mseto kuhusuhali hiyo.
Hizi hapa ni baadhi ya jumbe za maoni ya mashabiki hao;
@eunicendunge7412: "Maneno ya uthibitisho ambayo Kabi alikupa yanafaa na yatakuweka imara."
@praxidesmukhwana513: "Oh, Milly. Je, sasa unaweza kuwa na wakati wa pekee uliowahi kutaka? Pole mama❤ nakuhisi."
@emilymuchiku4543: "Mwenyezi Mungu awe pamoja na Milly na watoto wako
Hapo awali, Kabi alikuwa na hisia kali baada ya Milly kumpa zawadi ya iPhone 15 mpya na kutengeneza gari lake.
Kabi alishikwa na hisia baada ya mkewe kuisherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa mtindo.
Milly alimzawadia mumewe keki yenye mandhari ya iPhone na kumlipia likizo kwenda Malaysia. Pia alimletea iPhone 15 Pro Max mpya na akarekebisha gari lake, ambalo lilikuwa kwenye karakana kwa zaidi ya mwaka mmoja.