In Summary

• Hata hivyo msanii huyo alisema kwamba ziara yake Sirare iliyochochewa na nyama choma tamu ya mji huo wa mpakani ilitibuka baada ya mashabiki kumzingira kwa wingi.

Akothee akiendeshwa na Nelly Oaks.
Image: Facebook

Mjasiriamali ambaye pia ni msanii maarufu nchini Esther Akoth, ukipenda Akothee amekuwa na wikendi ya kufana katika maeneo ya mpaka kati ya Kenya n Tanzania.

Msanii huyo tangu Jumamosi amekuwa akipakia picha wakiwa wa aliyekuwa mpenzi wake Nelly Oaks katika miji ya Sirare mpakani lakini pia Tarime, mji ulioko Tanzania mpakani.

Akothee katika moja ya picha alionesha Nelly Oaks akiingia kuchukua usukani na kumwendesha kwenda mjini Sirare, jambo ambalo limezua uvumi kwamba huenda wamerudiana haswa baada ya penzi la Akothee na mpenzi wake Mzungu kusambaratika miezi 5 baada ya harusi ya kifahari.

Akothee alisema kwamba alifurahia kuendeshwa na Oaks ambaye amekuwa karibu naye kama mmoja wa wanafamilia wake kipindi ambacho alidai kwamba alikwenda nchini Uswizi na kukutana na kile alichokitaja kuwa hatari na kisichoweza kuzungumzika.

“Anaposema, I will drive, mimi sigwesi pinga Mkuu Nellyoaks. Kisha ninaanza kuimba, msichana mdogo ambaye hujui da ting, ninakufundisha da ting, unacheza wid da ting,” Akothee alisema huku akionesha Oaks akiingia kwenye usukani.

Hata hivyo msanii huyo alisema kwamba ziara yake Sirare iliyochochewa na nyama choma tamu ya mji huo wa mpakani ilitibuka baada ya mashabiki kumzingira kwa wingi.

“Leo tena tumeenda Sirare kwa sababu naitamani hiyo nyamchom ,lakini tulinyanyaswa na mashabiki hata kula tulishindwa 🤔🤔. Leo sikuhisi kama kuwa na walizni na sisi 💔. Chakula cha mchana kiligeuka kuwa vita, Kulikuwa na shabiki ambaye alikuwa tayari kwa vita, hivyo tukaondoka,” alisema.

Nelly Oaks na Akothee wamekuwa wakionekana pamoja katika siku za hivi karibuni licha ya kwamba waliweka wazi kuachana taribani miaka miwli iliyopita.

Nelly Oaks ambaye alikuwa meneja wa Akothee pia ana ukaribu wa kupigiwa mfano na wanawe msanii huyo.

View Comments