In Summary

• Khadija Kopa afunguka, wafuasi wetu wengi wamezama kwa Bongo flava jambo ambalo limefanya wasanii wengi na watunzi wa taarab kukata tamaa kwa maana hawana hela.

Khadija Kopa Mtunzi wa nyimbo

Muziki wa Taarab upo ila umeshuka bei, wengi wa wafuasi wamekita mizizi yao kwa nyimbo za kidijitali  za Bongo swala ambalo limefanya muziki wa taarab kusahaulika na kukosa wafadhili.

Ni kauli ya mwimbaji na mtunzi wa nyimbo za taarab Khadija Kopa.

"Wasanii wa muziki wa taarab wengi wao hali yao ni ya kichochole kwa kuwa muziki wa taarab umeshuka baada ya muziki wa Bongo kuchipuka kwa kasi, wafuasi wetu wengi wamezama kwa Bongo flava jambo ambalo limefanya wasanii wengi na watunzi wa taarab kukata taamaa kwa maana hawana hela",alisema Khadija Kopa.

Khadija Kopa alisimulia kuwa wasanii wa muziki wa taarab ambao wamesalia kushikilia muziki huo ni wale ambao majina yao yalichipuka kabla ya muziki wa Bongo kutawala.

Khadija Kopa aidha aliwasihi watunzi wa muziki wa taarab kushikana ili kufanya tamasha kwa pamoja.

'Najua wengi wa watunzi wamekata tamaa ila nawashauri tushikane pamoja ili muziki wetu huvutie jinsi ambavyo ulikuwa",alisema.

 

View Comments