In Summary

• Kupitia hadidhi zake za Insta,nyota huyo aliandika ujumbe mzito kwa wafuasi wake,akifanikisha maneno yao ya fadhili wakati wa kutengana.

• "Asante kwa wema wote ambao nimepata kwa kusambaza habari zangu za kuhuzunisha.maneno ya kutia moyo yanamaanisha zaidi kwangu kuliko nilivyotarajia,"

Lupita Nyong'o

Lupita Nyong`o anashukuru uungwaji mkono aliopokea kutoka kwa mashabiki wake baada ya kutangaza kutengana na mpenzi wake Salema.

Kupitia hadidhi zake za Insta,nyota huyo aliandika ujumbe mzito kwa wafuasi wake,akifanikisha maneno yao ya fadhili wakati wa kutengana.

"Asante kwa wema wote ambao nimepata kwa kusambaza habari zangu za kuhuzunisha.maneno ya kutia moyo yanamaanisha zaidi kwangu kuliko nilivyotarajia,"aliandika.

Kulingana na Lupita,amepokea barua kutoka kwa mashabiki wake zenye nyimbo,mashairi,vitabu na nukuu za kutia moyo ili kumsaidia kukabiliana na hali ya utengano.

Pia alitoa maneno ya kutia moyo yanayohusiana na uponyaji hasa kutoka kwa watu wanaojulikana.

Mnamo Octoba 19 mwigizaji huyo alishiriki kwenye Insta kuhusu kuumia kwake kufuatia kuvunjika kwa uchungu.

Alisema kwamba,licha ya ukweli kwamba kuna mambo mengi muhimu zaidi yanayoendelea ulimwenguni hivi sasa,ilikuwa lazima kwake kushiriki ukweli wa kibinafsi na kujitenga hadharani mwenyewe na mtu mbaye alisema hana uaminifu tena.

Nyong`o alisema kuwa alihamasishwa kuchapisha habari za kuvunja moyo kwa sababu ufahamu wa uzoefu  wake ungeweza kuwa wa muhimu kwa watu wengine.

"ufahamu wa uzoefu wangu unaweza kuwa muhimu kwa mtu mwingine huko inje anayepitia mtego wa mshtuko wa moyo ambaye yuko tayari kujaribu kutoroka kutoka kwa maumivu na kukosa hekima inayotokana nayo."

Siku moja kbla ya chapiho lake,yeye pamoja na Joshua jackson,ambaye alitalikiana hivi majuzi na mkewe Jodie Turner-Smith,walionekana huko Los Angeles na Nyong`o wakijitokeza pamoja na kukaa wakati wote wa onyesho hilo,huku akiwakaribisha marafiki zake na kuwatambulisha kwake.

View Comments