In Summary

• "Kwa hiyo 7 Heaven ni wazo la kuwezesha kurudisha taswria hiyo kwa Sanaa ya injili, ili tuweze kufanya kazi na watu watufuate wakijua kwamba huu ndio muongozo,” alisema.

Guardian Angel na vijana wake.
Image: Instagram

Msanii anayefanya vizuri kwa miziki ya kizazi kipya ya injili, Guardian Angel Alhamisi Oktoba 26 atazindua rasmi lebo yake ya muziki ambayo amekuwa akiijenga kwa muda, Seven Heaven Music.

Angel akizungumza na waandishi wa habari katika maandalizi ya siku hiyo kubwa, alisema kwamba tayari ameshawashika mkono vijana wawili walio na ndoto ya kuimba injili na wanafanya vizuri sana.

Msanii huyo aliweza kutaja sababu ya kuanzisha lebo ya injili wakati huu ambapo wengi wanahisi kwamba watu wengi wanasikiliza miziki ya kidunia.

“Tunaanzisha lebo ya injili kwa sababu kidogo ile taswira ambayo watu walikuwa nayo kuhusiana na muziki wa injili ilipakwa tope kidogo. Na hivyo ni vigumu sana kwa watu kufuata kitu ambacho wanahisi hakina mwelekeo wala uongozi. Kwa hiyo 7 Heaven ni wazo la kuwezesha kurudisha taswria hiyo kwa Sanaa ya injili, ili tuweze kufanya kazi na watu watufuate wakijua kwamba huu ndio muongozo,” alisema.

Msanii huyo alisema kwamba vijana hao wawili alioletewa kuwashika mkono na kufanya kazi nao kama vifungua mimba wa lebo hiyo hata hakuwa anawajua bali ni waliletwa kwake kutokana na kupendeza watu kwa jinsi walikuwa wanajitahidi katika video zao mitandaoni.

“Hawa vijana nililetewa na nikaambiwa kwamba wewe sasa kuwa mwelekezi na niliweza kuichukua kwa njia chanya. Kupitia kwa Sammy amekuwa mfano mzuri kwamba mimi nikipewa jukumu la kulea, jamaa anaingia mjini,” alisema huku akinukuu baadhi ya takwimu ambazo kijana huyo amepiga kwenye mitandao ya kijamii kufuatia kumchukua na kumpa nafasi ya kurekodi.

View Comments