In Summary

• Omondi kama kawaida alitoa rai kwa jamii yake ya mitandaoni ambao hawakumuangusha.

Eric Omondi
Image: Instagram

Kwa mara nyingine tena mwanaharakati Eric Omondi ameonesha upande war oho ya kubondeka kwa kunyoosha mkono wa msaada kwa mama ambaye mwili wa mwanawe ulikuwa umeshikiliwa makafani kwa Zaidi ya miezi minne.

Omondi alipopata simulizi ya huyo mama, alielezwa kwamab mwanawe alifariki miezi minne iliyopita na maiti yake imekuwa ikishikiliwa mochwari kwa muda huo wote kutokana na kutolipa bili.

Katika kipindi cha miezi minne, bili ya makafani ilikuwa imefikia shilingi milioni 2.8 ambazo zilikuwa mlima wa kuukwea kwa mama huyo aliyetaabika.

“Dylan Calmax alikufa miezi 4 iliyopita na hajazikwa bado kwa sababu ya bili ilioyoongezeka hadi Milioni 2.8. Mama yake Christine Mbale anahitaji kumpumzisha kijana wake ili aweze kupata Amani ya nafsi. AMEUMWA kiwewe,” Omondi alisema katika video ya kwanza akimuonesha mama huyo.

Omondi kama kawaida alitoa rai kwa jamii yake ya mitandaoni ambao hawakumuangusha, waliweza kuchanisha kiasi hicho cha pesa chini ya muda mfupi na kufanikisha mwili wa kinda huyo kuondolewa makafani na kupumzishwa.

Baada ya kupata sehemu ya kumzika katika makaburi ya Lang’ata na kununua jeneza, Omondi aliwataka wafuasi wake kujitutumua kwa mara nyingine ili kufanikisha safari ya mwisho ya mtoto Calmax.

“Tumenunua jeneza kwa kiasi kidogo tulichopokea na kuchimba Kaburi kwenye makaburi ya Langata. TUMEFANYA HIVYO GUYS!!! Hakuna nguvu kama nguvu katika UMOJA!!! Ni sisi Kwa Sisi. Tulifanikiwa kumpa Mtoto Dylan Mazishi ya heshima miezi 4 baada ya kufariki. Tulifanikiwa kumpa Mama yake Christine Kaluki UTULIVU na AMANI. SHUKRANI KWA WOTE ALIYECHANGIA!!! MUNGU AKUBARIKI,” Omondi alisema katika video nyingine wakimzika mtoto huyo.

 

View Comments