In Summary

• Alikiba na Tommy Flavour waliachia ngoma hiyo kama mwezi mmoja hivi uliopita na wiki mbili zilizopita waliweza kuachia video rasmi.

• Wimbo huo una mdundo Fulani wa Amapiano kwa mbali ambayo imechanganywa na midundo ya Bongo Fleva.

Alikiba na Tommy Flavour
Image: Screengrab

Msanii Alikiba na Tommy Flavour ambaye yuko chini ya lebo yake ya Kings Music hawashikiki tena.

Hii ni baada ya video kuibuka ikiwaonesha wachezaji wa timu ya Liverpool nchini Uingereza wakishiriki mazoezi huku wakifurahia kuisikiliza ngoma yao ya hivi majuzi, Huku.

Video hiyo iliibuliwa na mchambuzi nguli wa maswala ya spoti kutoka Clouds FM, Shaffih Dauda ambaye kupitia ukurasa wake wa Instagram siku moja iliyopita, alishiriki video hiyo.

Video hiyo inawaonesha mastaa kama Anorld Alexander na Mohammed Salah wakiwa kwenye chumba cha kufanya mazoezi ya kunyanyua vyuma cha timu hiyo huku wimbo unaosikika nyuma ukiimba ukiwa ni ‘Huku’.

Ngoma ya ‘HUKU’ ya @officialalikiba na @tommyflavour ikichezwa wakati wachezaji wa Liverpool wakiwa mazoezini. Ipo katika channel rasmi ya YouTube ya Liverpool!” Dauda aliandika kwenye klipu hiyo fupi.

Alikiba na Tommy Flavour waliachia ngoma hiyo kama mwezi mmoja hivi uliopita na wiki mbili zilizopita waliweza kuachia video rasmi.

Wimbo huo una mdundo Fulani wa Amapiano kwa mbali ambayo imechanganywa na midundo ya Bongo Fleva.

“Huku, nishike huku babe nishike huku,” sehemu ya kibwagizo cha wimbo huo kinaimba.

Walipotoa audio ya ngoma hiyo nak uiambatanisha na mishororo kwa njia ya video isiyo rasmi, wimbo huo ulijizolea watazamani Zaidi ya milioni 1.6 ndani ya mwezi huo mmoja lakini pia tangu kuachia video rasmi, siku 12 sasa wimbo huo umegonga views Zaidi ya laki 6.

View Comments