In Summary
  • Mtule amesema kwamba polisi wanaendelea kuchunguza kisa hicho ili kuwakamata waliohusika.

Msanii wa nyimbo za injili Nchini Mwana mtule kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram amekanusha na kutupilia mbali madai kwamba ameaga dunia.

Hii ni baada ya kuripotiwa kuwa msanii huyo ameaga dunia.

Hata hivyo ameweka wazi kwamba alipewa sumu alipokuwa kwa rafiki yake eneo la Rongai.

Mtule amesema kwamba polisi wanaendelea kuchunguza kisa hicho ili kuwakamata waliohusika.

"Habari Familia 🙏😞 Haya sio kutafuta kiki tafadhali acheni kuniandikia R.I.P

Sijafa, namshukuru Mungu kwa kuokoa maisha yangu Nililishwa sumu Mahali pa Marafiki, eneo la RONGAI."

Aliongeza;

"Nitazungumza nanyi hivi punde niwaeleze kilichotokea maana Sasa bado sijisikii vizuri 🙏🙏 Mungu awabariki wote

Bado niko hai 🙏🙏🫂...Polisi bado wanaendelea na uchunguzi Kwa washukiwa 🙏🫂🫂."

Wasanii wengi Nchini wanafahamika kwa kutafuta kiki kutoka kwa mashabiki ili kusukumavibao vyao ilhali Mtule amekana na kusema kwamba sio kiki anatafuta.

 

 

 

 

View Comments