In Summary

• “Unapopata muda wako utumie vizuri. Mungu amekupa wakati, usimfanye akaona kwamba kampa wakati mtu asiyestahili." alisema.

Diamond Platnumz.
Image: Screengrab

Msanii na mjasiriamali Diamond Platnumz ameweka wazi ndoto yake ya maisha ambayo angependa kuyaishi pindi baada ya kustaafu kuiba muziki.

Diamond ambaye katika kipindi cha siku za hivi karibuni amekuwa akizunguka katika mataifa mbali mbali kwa ajili ya shoo na mjumuiko wa kifamilia, alisema kwamab analazimika kufanya hivi kwani si muda wote atakuwa na muda huo milele.

Diamond alitua katika uwanja wa Kahama nchini Tanzania ikiwa ni saa chache baada ya kutumbuiza jijini Nairobi katika tamasha la Oktobafest na alisema kwamba kesho pia atakuwepo nchini Marekani kwa ajili ya mitikasi yake.

Msanii huyo alisema anahakikisha anautumia muda wake kwa sasa ili siku zijazo aje kustarehe kama msanii nguli wa HipHop kutoka Marekani, Jay Z ambaye kwa sasa anavuna kutokana na yale aliyowekeza katika muziki siku za nyuma.

“Unapopata muda wako utumie vizuri. Mungu amekupa wakati, usimfanye akaona kwamba kampa wakati mtu asiyestahili. Mfanye Mungu awe proud aone kwamba amekupa nafasi na wewe umeitumia vizuri, utendee haki, husisha watu. Lakini yaani nafasi hiyo itumie kwa namna chanya as much as you can,” Diamond alisema.

“Utafika muda nitapumzika nita rest. Sitaimba muziki milele, kuna muda nataka tu nitulie nifurahie matunda yangu kama Jay Z. sasa hiki kipindi cha kumalizia kukusanya nakusanya kwelikweli,” Diamond aliweka wazi kwa nini amekuwa na uchu wa kuruka kutoka nchi moja kuelekea nyingine bila kupata muda wa kupumzika.

Itakumbukwa msanii huyo kwa karibia miezi miwili sasa amekuwa katika mwendelezo wa tamasha la Wasafi Festival katika mikoa mbali mbali nchini Tanzania.

Kando na tamasha hilo, Diamond pia amepata muda wa kutembelea familia yake nchini Afrika Kusini kukaa na wanawe na Zari, kabla ya kurudi nchijni Tanzania kuendelea na Wasafi Festival na pia kwenda Rwanda kwa ajili ya shoo ya uzinduzi wa tuzo za Trace, kuruka hadi Kenya na kurudi Tanzania kwa tamasha lake, yote hayo ndani ya mfululizo wa siku chache.

 

View Comments