In Summary

•Wakati wa uzinduzi wa duka la bintiye, Kajala aliweka rekodi sawa kwa nini Marioo alikuwa akimpongeza mpenzi wake.

•Paula alijibu kutoka upande mwingine akiwaambia wanaomdhania  kusubiria  mimba wanaoyoizungumzia ikiwa ipo.

Frida Kajala na paula Picha:YouTube/Screen Short

Mwigizaji Fridah Kajala amezungumzia madai ya binti yake Paula kuwa na ujauzito wa mwimbaji wa Bongo Marioo.

Madai hayo yaliibuka baada ya Marioo kuweka posti la kumpongeza Paula. Hata hivyo hakuweka wazi sababu ya kumpongeza.

“Hongera sana mpenzi wangu ❤️ @therealpaulahkajala proud of you 🙈 I can’t wait,” Marioo alishiriki kwenye Instagram.

Hata hivyo, wakati wa uzinduzi wa duka la bintiye, Kajala aliweka rekodi sawa kwa nini Marioo alikuwa akimpongeza mpenzi wake.

“Omari alipost kama kumpongeza Paula kwa ajili ya kufungua duka lakini kwa kuwa binadamu tayari wanadhania kuwa  Paula ana uja uzito, kwa hilo wamejijibia wenyewe. Sisi inabidi tuwaangalie tu kwa kuwa wao ndio wanaongea lakini sisi tunajuwa Omari alikuwa anazaungumzia duka,” mwigizaji huyo aliwaambia waandishi wa habari.

Paula alijibu kutoka upande mwingine akiwaambia wanaomdhania  kusubiria  mimba wanaoyoizungumzia ikiwa ipo.

“Nikiwa nayo mtaona kwa sababu mimba haifichiki,” Paula alisema.

Ili kusisitiza zaidi suala hilo, Kajala alisema kuwa binti yake atapata ujauzito kwa wakati wake unaofaa.

“Vijijini watu wanajifungua hata wakiwa na umri wa miaka kumi mpaka  kumi na minne, kwa hiyo msitake kuhukumu kwa sababu paula anaonekana mitandaoni. Yeye mwenyewe akiona anataka kujifungua  mwacheni ajifungue,” alisema.

Aidha, Kajala alimsifu Marioo akisema kwamba ana heshima. Kuhusu ndoa yake na Paula, alisema pia kwamba alikuwa bado amjulishe babake Paula.

“Sijaongea naye kwa muda mrefu. lakini kuna vitu vinavyoendelea lazima nimshirikisha yeye ni baba,” alisema.

View Comments