In Summary

• Katika video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii, nyota huyo aliyeshinda tuzo ya Grammy alitumbuiza kwa mtindo huru wakati wa mazoezi yake ya hivi majuzi ya bendi.

Burna Boy
Image: Instagram

Msanii kutoka Nigeria, Burna Boy amezua mjadala pevu katika mitandao ya kijamii hivi majuzi baada ya kutoa sababu ya kimsingi iliyomfanya kukataa shoo ya dili nono ya kutumbuiza katika jukwaa moja jijini Dubai.

Burna Boy alisema kwamba alikuwa ameahidiwa dola milioni 5 sawa na shilingi milioni 755 pesa za Kenya ili kutumbuiza kwenye shoo hiyo ya Dubai lakini aliikataa baada ya kuambiwa kwamba kulikuwepo na kipengele kilichonuia kumzuia kutumia kileo chochote wala kuvuta bangi wakati anatumbuiza kwenye jukwaa.

Ikumbukwe msanii huyo amekuwa akionekana akijivinjari na fegi zake jukwaani akitumbuiza huku akiachia moshi kutoka mdomoni na puani kwa raha zake na za mashabiki wake.

Katika video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii, nyota huyo aliyeshinda tuzo ya Grammy alitumbuiza kwa mtindo huru wakati wa mazoezi yake ya hivi majuzi ya bendi.

Akiwa anafanya mitindo huru, Burna Boy alitaja jinsi alivyokataa ofa hiyo kwa sababu kuvuta "unyasi" huko Dubai ni kinyume cha sheria. Alidai kuwa dola milioni 5 hazikuwa muhimu kwake kwa sababu aliepuka hali ambazo hangeweza kumpa uhuru wa kuvuta "unyasi" wake.

Wakati huo huo, huko Dubai, uvutaji sigara ni kinyume cha sheria chini ya sheria za Emirate.

Kumbuka kwamba mwimbaji mashuhuri wa Uingereza Ed Sheeran alivutia hisia za Wanigeria siku za hivi majuzi kwa ufichuzi aliotoa kuhusu mwimbaji wa Afrobeats Burna Boy.

Katika mahojiano yake, msanii huyo wa Uingereza alisimulia tukio la mara moja ambalo alisema katika maisha yake ya muziki, hajawahi kutana na msanii anayevuta bangi kwa Zaidi kama ambavyo Burna Boy alikuwa anafanya wakati wanashughulikia kolabo yao.

View Comments