Mamake Dvoice amsifia Diamond pakubwa baada ya kusaini mwanawe WCB Wasafi
Wasafi Ndio Lebo bora zaidi kwa wanamuziki Mamake Dvoice asema
• Mzazi Huyo alifunguka huku akisema kuwa alipata muda wa maongezi na msanii Diamond huku akisema kuwa kauli ya Diamond kwake alimtaka awe jasiri kwa kuwa mwanawe atasemwa kwa mazuri na mabaya
Siku chache baada ya msanii mpya wa Bongo Dvoice kutambulishwa rasmi kwenye Lebo ya Wasafi chini ya uongozi wa Diamond Platnumz mamake mzazi amejitongeza hadharani huku akimuminia sifa tele Diamond.
"Nimemjua Msanii Diamond kwa muda mchache kwa jinsi alivyo na roho ya utu na mpenda maendeleo kumtabulisha Dvoice kwa Lebo yake ni jambo nitaishi kukumbuka kwa maisha yangu yote kwa kuwa yuko chini ya nyota shupavu Diamond,"alisema.
Mzazi Huyo alifunguka huku akisema kuwa alipata muda wa maongezi na msanii Diamond huku akisema kuwa kauli ya Diamond kwake alimtaka awe jasiri kwa kuwa mwanaye atasemwa kwa mazuri na mabaya.
"Diamond aliniambia kwa kuwa mwanangu ameingia kwenye Lebo kubwa niwe tayari kwa vita vya mitandao masengenyo na taarifa nyingi za kuudhi,"alisema mamake D Voice.
Mamake Dvoice alisema hayo baada ya kufanyiwa mahojiano ya moja kwa moja na wanablogu wa mitandao huku akimtaka mwanaye D voice kujituma vilivyo ndani ya Wasafi kwa kuwa alitia saini baada kupita maelezo yote.
"Namtakia mwanangu kila laheri ila namuomba afanye bidii zake zote wasafi kwani ndio lebo tu ambayo anaweza kubadilisha maisha yake,"alisema.