In Summary

• Umati ambao pia ulikuwa umekusanyika ulikashifu hatua ya afisa huyo wa kaunti kwa kukosa huruma kwa kijana huyo.

Mchuuzi amwagiwa njugu na kanjo.
Image: Instagram//screengrab

Kila siku ni siku mpya ya Wakenya kupokea taarifa za kutia huruma kutokana na visa vya kukera vinavyotekelezwa na maafisa wa kaunti maarufu kama kanjo.

Kwa mara nyingine tena Wakenya katika mitandao ya kijamii wamegubiwa na kero kwa kanjo baada ya video moja kuenezwa ikimuonesha kijana mwenye umri wa makamo akitiririkwa na machozi asiweze kufarijika baada ya kanjo kudaiwa kumwaga ndoo yake ya njugu.

Jijini Nairobi, ni kawaida kukutana na vijana wanaojaribu kutafuta riziki kwa kuchuuza vyakula vya haraka kama njugu karanga, mayai chemsha na vingine mitaani.

Kijana huyo aliyerauka mapema kuchuuza karanga kwa wapiti njia alipatana na kasa huo baada ya kile kilidaiwa ni kukutana na askari wa kanjo ambaye alimpokonya ndoo yake na kuzitapakaza zote kwenye sakafu ya lami.

Katika video ambayo imesambaa kwa kasi, kijana huyo asiyejiweza alionekana akilia huku akiwa amemshikilia na askari wa kaunti.

Umati ambao pia ulikuwa umekusanyika ulikashifu hatua ya afisa huyo wa kaunti kwa kukosa huruma kwa kijana huyo.

Video hiyo ya kutia huruma ilimfikia mwanaharakati wa kibinadamu Eric Omondi ambaye aliapa kumtafuta ili kumweka katika mpango wa kuchangishiwa pesa na kujinasua kimaisha jijini.

“Wakimwaga Tunaokota...Wakibomoa TUNAJENGA!!! Namtafuta huyu Kijana kama una namba yake tafadhali comment nayo au DM ME🙏🙏. Lakini kumbuka WAKATI WETU UNAFIKA!!!!!” Omondi alisema.

View Comments