In Summary

•Mchekeshaji huyo alisifia taifa la Kenya kwa kuwa ni taifa ambalo inakubali sanaa na kufanya iwe rahisi kwao kwani wana huru wa kuadaa sanaa mahali popote nchini

Image: INSTAGRAM// NJUGUSH

Mchekeshaji Njugush amewasifia Wakenya kwa mchango wao wa kuunga mkono sanaa ya waudaji maudhui wa humu nchini kwa kulifikisha kwa kiwango cha juu.

Mchekeshaji huyo na ambaye alifanyiwa mohojiano ya moja kwa moja na mwanablogu wa mtandao alipiga vikali uvumi ambao uenea kwamba Wakenya wengi hawapendelei sanaa ya humu nchini.

"Wengi husema kuwa Wakenya wengi hawapendelei sanaa ya humu nchini ila mimi napigana na jambo hilo kwa kuwa wafuasi wengi ambao ufuatilia sanaa zetu ni wakenya na wengi ufanya juhudi kuakikisha sanaa imekuwa  kiwango cha juu na ya  kupendeza,"alisema Njugush.

Kulingana naye Wakenya kupita  kutazama sanaa kwenye mitandao umekuwa ni mchango mkubwa kwa waunda maudhui kwani wengi ulipia zaidi ya elfu tatu wakati wanapoadaa maonyesho ya sanaa kwenye ndani ya ukumbi.

"Sanaa ya kenya inaugwa mkono na wengi ikiwemo sanaa ya mitandao ya kijamii na pia sanaa ambayo uandaliwa kwenye makavazi wengi wa wakenya ulipia zaidi ya elfu tatu kwa maonyesho ya moja kwa moja jambo ambalo inachangia pakubwa kukua kwa sanaa.

Mchekeshaji huyo kwenye mahojiano hayo alisifia taifa la Kenya kwa kuwa ni taifa ambalo inakubali sanaa na kufanya iwe rahisi kwao kwani wana huru wa kuadaa sanaa mahali popote nchini.

 

View Comments