In Summary

• Wamekuwa pamoja tangu Mulamwah alipoachana na Carrol Sonie mwishoni mwa mwaka 2021.

Mulamwah na Ruth K
Image: Facebook

Mapema wiki hii mitandao ya kijamii ilisisimuka kufuatia taarifa njema kutoka kwa Mulamwah na mpenzi wake ambaye amekuwa akikana uhusiano wao kwa Zaidi ya mwaka mmoja – Ruth K.

Mulamwah na Ruth K, waliweka wazi kwa mashabiki wao wa mitandaoni taarifa ya kutarajia mtoto wao wa kwanza pamoja, ikiwa ni kutoka Oktoba 2023 Mulamwah alipoonekana naye kwa mara ya kwanza, saa chache baada ya kuachana na babymama wake Carrol Sonie.

Mulamwah na Ruth K kila mmoja alipakia picha mbalimbali za kuthibitisha ujauzito kaitka kurasa zake mitandaoni lakini pia waliziambatanisha na video na maelezo ya kumshukuru Mungu kwa safari yao ya mapenzi.

Baadae watu mbalimbali walianza kufanya uhariri wa picha hizo wakihariri sura na vichwa kuonesha sura za watu tofauti, jambo ambalo lilionekana kumkera Mulamwah.

Mchekeshaji huyo alikwenda mitandaoni na kutoa onyo kwa wanaofanya uhariri huo, akitaja gharama ya juu ambayo photoshoot hiyo ilichukua.

Alaaaa yaani photoshoot yetu ya 150k ndio mnachezea ivi jameni ” Mulamwah aliandika akionesha moja ya picha hizo zikiwa zimehaririwa na kupandikizwa sura tofauti.

Awali mchekeshaji Eddie Butita pia alitoa maoni yake katika moja ya picha ya Mulamwah na Ruth K ambayo ilihaririwa na kuwekwa kichwa chake.

Mulamwah alianza mahusiano na Ruth K mwishoni mwa mwaka 2021, saa chache tu baada ya kuweka taarifa bayana kwamba yeye na mamake mtoto wake – Carrol Sonie – walikuwa wamefika mwisho wa kushindwa kufikia maelewano ya kuendeleza uhusiano wao.

Kilichofuata ni kutupiana lawama kutoka kwa pande zote mbili na kwa wakati mmoja Mulamwah akiweka wazi kwamba Ruth K hakuwa mpenzi wake bali ni msanii aliyesainiwa chini ya Mulamwah Entertainment.

Aliendeleza kumtambulisha kama ‘Bestie’ na kufutilia mbali uwezekano wa uhusiano wa kimapenzi licha ya dalili zote kuonesha kwamba kulikuwepo na kina kirefu cha mapenzi kati yao.

Hata hivyo, hakuna marefu yasiyo nan cha, wiki hii dunia nzima ilifahamu kwamba wawili hao ni wapenzi baada ya kushindwa kuficha mimba na kuamua kumwaga mtama kwenye kuku wengi.

View Comments