In Summary

• Esma alimtakia kheri njema Zuchu lakini akamtambulisha kama ‘mdogo wangu’ jambo ambalo wengi walihoji mbona si wifi.

Zuchu na Esma Platnumz
Image: Facebook

Novemba 22 huwa ni siku ya msanii wa WCB Wasafi, Zuchu kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Wakati anasherehekea, pia mashabiki wake walimsherehekea wengine kwa kupakia picha zake na kumtakia heri njema ya miaka 30.

Mmoja wa waliochapisha picha yake ni Esma Platnumz, dadake na Diamond Platnumz ambaye amekuwa akitajwa kuwa kando na Zuchu kuwa mwajiri wake katika lebo, pia ni mpenzi wake.

Lakini ujumbe ambao Esma aliandika kwenye picha hiyo ulizua maswali mengi kutoka kwa mashabiki wengi ambao walihoji kwamba huenda ujumbe huo uko na maana ya kile kilichosababisha Zuchu kum’unfollow Diamond kwenye Instagram.

Esma alimtakia kheri njema Zuchu lakini akamtambulisha kama ‘mdogo wangu’ jambo ambalo wengi walihoji mbona anamuita mdogo wake badala ya kumtambua kama wifi wake kwa kuwa ni mpenzi wa kakake, Diamond.

Heri ya kuzaliwa Mdogo wangu @officialzuchu Mzanzibar Kinuna 🤭🤣 maisha marefu Dogo kesho nakuja kukumwagia majiiiiii mapema home,” Esma aliandika.

Zuchu pia naye katika kujibu kwake, kulihakiki kabisa kwamba Esma huenda hakupotelewa na maneno, kwani naye alimshukuru kwa kumtaja kama ‘dadangu’ badala ya wifi.

“Kwa nini kinuna Asante my sister ️ maji na zawadi,” Zuchu alisema.

Sasa mashabiki wanaofuatilia kwa ukaribu kile ambacho kimekuwa kikiendelea baina ya Zuchu na Diamond katika siku za hivi karibuni tangu aonekane anakula bata na babymama wake, Tanasha Donna, walikuwa wa haraka kutambua ‘kosa’ hilo na kuhoji kama uwifi umesambaratika baina ya Zuchu na Esma.

Haya hapa ni baadhi ya maoni ya mashabiki wakihoji kuhusu suala hilo.

“Kwa hiyo hamna anaesema hbd shemejiiiii wala wifiii 😂sio poa jamani,” Lisa Malelo.

“mmmmmh nikajua utamuita wifi ngoja nilaze komwe langu” Coxdawayao.

“Ndo kusema hutaki kumuita wifio eh” Nabusimbasportslady.

“Mdogo wako au ni wifi yako mbona unajizima data😂😂😂” Aminajuma.

Itakumbukwa ni hivi majuzi tu ilibainika kwamba Zuchu amesitiza urafiki na Diamond katika mtandao wa Instagram, jambo ambalo liliwafanya wengi kuhisi huenda kuna tatizo katika mapenzi yao.

View Comments