In Summary

• Vera alisema kuwa hali yake si sawa huku akiomba msaada wa maombi kutoka kwa mashabiki wake. 

• “Sijiskii vizuri,nikumbukeni nyote katika maombi,”

Sosholaiti Vera Sidika
Image: INSTAGRAM

Katika chapisho lake la hivi punde kwenye ukurasa wake wa insta,Vera alisema kuwa hali yake si sawa huku akiomba msaada wa maombi kutoka kwa mashabiki wake.

“Sijiskii vizuri,nikumbukeni nyote katika maombi,” aliandika.

Vile vile alisema kuwa huenda akaondoka mitandaoni kwa muda mpaka pale atakapo pata nafuu.

“Nimekuwa nje ya mtandao na nitakuwa nje ya mitandao ya kijamii kwa muda hadi pale nitakapojiskia vizuri,nawapenda wote,”alieleza.

Wiki chache zilizopita,Sidika alitangaza kujiondoa katika hafla ya tafrija ambayo aliratibiwa kutokea huko Mwea kaunti ya Kirinyaga.

Sidika ambaye alikuwa ameratibiwa kutokea kwenye hafla hiyo pamoja na wasanii na watu wengine maarufu Zaidi ya watano kutoka tansia ya burudani humu nchini, alitangaza hilo siku mbili tu kuelekea siku ya tukio.

Alidokeza kwamba asingeweza kutokea kwa kile alichokitaja kwamba tafrija hiyo imepangiwa pia msanii Brown Mauzo, ambaye ni mpenzi wake wa zamani ambaye wana watoto wawili pamoja.

Vera alisema kwamba aligundua hafla hiyo inatangazwa kwa njia ambayo wenye tafrija wanataka kutumia mzozo wa kuachana unaoendelea baina yake na Brown Mauzo ili kufaidika, na hivyo hatoweza kukubali hilo kutokea kwa kuhusisha chapa yake na biashara ya aina hiyo.

“Imekuja kwa mawazo yangu kwamba baadhi ya watu binafsi na blogs wanatangaza utendaji fulani kati yangu na Ex kule Mwea. Ningependa kuwafahamisha mashabiki wangu na umma kwa ujumla kuwa aina hii ya utangazaji ni ya kupotosha na ni ya udanganyifu iliyoundwa katika muundo ili kufaidika kutokana na hali ya familia yangu binafsi. Tafadhali kumbuka kuwa sitahudhuria au kufanya maonyesho katika bustani za mtendaji wa Jami, Mwea,” Sidika alitangaza.

View Comments