In Summary

• Katika mazungumzo na wanablogu,Dem wa FB alisema kuwa jinsi ambavyo uchumi unaendela kupaa,hawezi jiingiza kwenye mahusiano na hasa wanaume wa Kenya.

• “Siwezi kuchumbiwa na wanaume wa Kenya wenye ambao bado wanahangaika,vitu zikipanda bei wanaenda maandamano,na ndoa je watafanya nini?”

Dem wa FB
Image: Instagram

Muunda maudhui maarufu anayetambulika kama Dem wa FB,ameibua hisia na baada ya kusema kwamba hawezi ingia kwenye mahusiano na wanaume wa Kenya.

Katika mazungumzo na wanablogu,Dem wa Fb alisema kuwa jinsi ambavyo uchumi unaendela kupaa,hawezi jiingiza kwenye mahusiano na hasa wanaume wa Kenya ambao alisema wanakwaruzwa na hali ngumu ya uchumi.

“Siwezi kuchumbiwa na wanaume wa Kenya wenye ambao bado wanahangaika,vitu vikipanda bei wanaenda maandamano,na ndoa je watafanya nini?”alisema kwa ujaziri.

Alisema afadhali asalie bila kuguswa na mwanaume yeyote kwa maisha ya mbeleni.

Dem wa FB alisema kuwa mojawapo ya mambo ambayo hupelekea ndoa kuvunjika ni kwa sababu wanaume wanashindwa kukidhi mahitaji ya wake zao.

“Mwanamke atunzwi na maombi mwanamke anatunzwa na pesa,”alisema.

Katika hayo mazungumzo alijibu madai ya kutaka kuchumbiwa na mmoja wa wafuasi wa Azimi anayetambulika kama KImbikimbi na kusema kuwa awezi akafikia level yake.

“Kimbikimbi  sio aina yangu yeye ni mweusi na mimi ni mweusi,si tutapata watoto giza , yeye mwenyewe anavaa ndala za mia,na nguo zake mwenyewe ni za gikomba,mimi atawza kunitunza,?alisema.

Alieleza na kusema kuwa msimamo wake nkali wa kutochumbiana na wanaume kwa sasa unatokana nay eye kuwa bikira ambaye ajajihusisha  na mwanaume yeyote kimapenzi.

“Nimeweka msimamo kwa sababu kwa ulimwengu wa sasa ni nadra sana kumpata msichana akiwa bikira,”alieleza.

Aidha alieleza kuwa wanaume wanaepuka kumchumbia kwa sasabu  hana makalio makubwa akisema kwamba wasubiri tu kuna mambo yako motoni yaiva ambayo yatafanya wanaume kumgangania.

View Comments