In Summary

• Hata hivyo alisisitiza kwamba shil9ngi bilioni 4 si kitu kwa Diamond japo kwamba kuibiwa kwazo kulififisha ndoto yake tena kununua ndege ya kibinafsi.

Diamond na Baba Levo
Image: Facebook

Chawa na mtunza siri mkuu wa Diamond Platnumz, Baba Levo ameonesha kwamba bado kitendo cha Diamond kutapeliwa shilingi za kitanzania Bilioni 4 kimasihara katika mchakato wa kununua ndege ya kibinafsi bado kinamuumiza sana.

Levo katika kipindi cha Refresh kwenye Wasafi, alibainisha kwamba yeye anazidi kumshawishi na kumpa msukomo Diamond kwamba wasije wakaacha suala hilo likaenda hivi hivi hata kama liko mikononi mwa sheria.

Alifichua kwamba anafikiria kupiga debe mali yake yote ili kuanza kuhangaika kumtafut mtapeli huyo aliyemharibi ndoto ya kupanda ndege ya kibinafsi.

“Kuna watu ambao wameshamtendea mabaya Diamond Platnumz, wamechukua Zaidi ya bilioni 4 ambazo tulikuwa tunategemea tupande na sisi private jet ya mzee wake, Diamond ni mzee wangu, sasa hiyo ndoto imeuawa. Sasa nasema hivi, kama ni mswahili tutaonyeshana hapa hapa Kiswahili na wale ambao ni wazungu tutawafuata huko,” alisema akijaribu kujichanganya katika lugha ya Kiingereza.

Hata hivyo alisisitiza kwamba shil9ngi bilioni 4 si kitu kwa Diamond japo kwamba kuibiwa kwazo kulififisha ndoto yake tena kununua ndege ya kibinafsi.

“Diamond ndio msanii wa Tanzania tajiri kwa hiyo hamkuchukua chochote, tutawapata na mtaona chenye tutawafanyia, tutaona. Bilioni 4 ni kama anayeramba asali kwenye pipa, utamalizaje asali kwa kuiramba? Niko tayari niuze vitu vyangu vyote, magari na hata nyumba nitafute hela niende huko kwenye mwizi huyo yuko,” aliongeza.

Mwezi mmoja uliopita, Diamond alifichu kwamba mashabiki wake hawajapata kuona akiruka na ndege yake ya kibinafsi kama alivyowaahidi mwaka jana.

Alifichua kwamba alitapeliwa kiasi hicho kikubwa cha hela lakini pia akasema kuwa mamlaka husika zilikuwa zinalifanyia kazi suala hilo.

View Comments