In Summary

• Lakini kukutana kwao kulichukua mkondo tofauti baada ya kuanza kama mzaha na kuishia kupapurana japo kwa mzaha.

• Mashati yalianza kuchanika pale Mwijaku alipomwambia Baba Levo kwamba amemuombea fursa kwa Harmonize kumuandikia wimbo.

Mwijaku na Baba Levo.
Image: Screengrab

Machawa Baba Levo na Mwijaku walifikia hatua ya mwisho kabisa ya kuchambana baada kukutana katika hafla ya kuiaga timu ya Simba SC.

Wawili hao baada ya muda kuchambana kila mmoja akimtupia mwenzake povu zito kwenye waandishi wa habari za mitandaoni, hatimaye Simba SC iliwakutanisha katika kile walidai kwamba wanakwenda Uchina pamoja.

Lakini kukutana kwao kulichukua mkondo tofauti baada ya kuanza kama mzaha na kuishia kupapurana japo kwa mzaha.

Mashati yalianza kuchanika pale Mwijaku alipomwambia Baba Levo kwamba amemuombea fursa kwa Harmonize kumuandikia wimbo.

Ikumbukwe Baba Levo ambaye ni mwandani kabisa wa Wasafi na Diamond Platnumz amekuwa akiwakosoa wasanii Harmonize na Alikiba kwa karibia kila kitu – wasanii ambao mara nyingi Mwijaku amekuwa akiwasifia pakubwa na kumkejeli Diamond.

“Mzuie huyu nitamuua, huyu ananiudhi kwa sababu ya kitu kimoja, huyu ni kijana wa hovyo, nimemtafutia nafasi kwa Harmonize amwandikie nyimbo, Harmonize amemuandikia halafu hataki kutoa shukrani, sema ahsante unakosea,” Mwijaku alisema huku wakiendelea kupapurana.

Hata hivyo, Baba Levo alikanusha kuandikiwa wimbo akisema kwamba hawezi andikiwa wimbo na Harmonize akidai kwamba yeye mwenyewe ameshindwa kujiandikia nyimbo za kuvutia kwa mashabiki.

“Harmonize aniandikie wimbo mimi, ashindwe kujiandikia mwenyewe nyimbo na amezidiwa na Dvoice,” Baba Levo alisema.

View Comments