Koffi Olomide azuru Radio Jambo, na kuahidi shoo ya kumezea mate
Tikiti za mapema zinauzwa kwa Sh6,000, watakaonunua getini watalipa Shilingi 7,500 na VIP watalipa Sh25,000.
• Mwanamuziki huyo wa rhumba/soukous alisema anashukuru kwa kupata fursa ya kurejea Kenya na kuonyesha kipawa chake.
Msanii maarufu kutoka DRC Koffi Olomide almaarufu Le Grand Mopao Mokonzi alitua Nairobi Desemba 6 kwa ajili ya tamasha la amani lililoandaliwa na Radio Africa Events.
Koffi atatumbuiza pamoja na wasanii wengine mnamo Desemba 9, 2023, kwenye Ukumbi wa ASK Dome, eneo la mainyesho ya Kilimo ya Nairobi.
Tikiti zinauzwa, na mashabiki wanaweza kuzipata kupitia ticketyetu.com.
Tikiti za mapema zinauzwa kwa Sh6,000, watakaonunua getini watalipa Shilingi 7,500 na VIP watalipa Sh25,000.
Mwanamuziki huyo wa rhumba/soukous alisema anashukuru kwa kupata fursa ya kurejea Kenya na kuonyesha kipawa chake.
"Nina furaha zaidi, na siwezi kusubiri kuwa jukwaani na kutumbuiza watu wa Kenya. Nina furaha sana kuwa hapa," alisema.