In Summary

• Afro alianza kwa kuwatambulisha wachekeshaji waliosalia kutoka kwa vipindi vya ucheshi vya miaka ya nyumba.

Wachekeshaji
Image: Screengrab

Sherehe za kuadhimisha miaka 60 ya uhuru wa Kenya mwaka huu zilifanyika kwa njia ya kipekee katika uwanja wa Uhuru Gardens.

Katikac sherehe hizo, kando na wasanii wa muziki, pia wachekeshaji wa ezni za zamani za ya sasa walipata nafasi ya kumtumbuiza rais kwa vichekesho vyao adimu.

Mtafsiri wa filamu za kigeni kwa muda mrefu humu nchini, DJ Afro aliwaongoza wavhekeshaji hao wote kutoka vizazi vya nyuma na vya sasa kumfurahisha rais na wageni wa heshima walioalikwa.

Afro alianza kwa kuwatambulisha wachekeshaji waliosalia kutoka kwa vipindi vya ucheshi vya miaka ya nyumba kama vile kipindi cha Vitimbi chao Mama Kayai, Mzee Ojwang’ kabla ya ujio wa kipindi cha Vioja Mahakamani.

Mchekeshaji Makokha na mwenzake Ondiek Nyuka Kwota waliwakilisha kipindi cha Vioja Mahakamani kwa kumchekesha rais ambapo walitaniani kuhusu vazi la kizalendo, Makokha akimwambia mwenzake kuwa aache kubisha kwani yeye ni mzalendo Zaidi kumliko kutokana na kuvaa tai ya rangi za bendera ya Kenya.

Baadae pia Afro alimtambulisha mchekeshaji ambaye pia ni mtangazaji wa redio, Jackie Nyaminde ambaye alikuwa anaigiza kama mke wa Papa Shirandula kwenye runinga ya Citizen kwa jina Wilbroda.

Wilbroda alimchekesha rais kwa kumuuliza kwamba kwa vile mume wake – Papa Shirandula – ameshafariki, yeye sasa yuko single na kumtaka rais Ruto kumtafutia mwanamume yeyote hata kama ni kutoka kwa baraza lake la mawaziri.

Afro pia aliwatambulisha wengine kama vile Inspekta Mwala ambaye ameigiza runingani kwa muda mrefu katika vipindi vingi, lakini pia akautambua mchango mkubwa wa Churchill katika ujio wa kizazi kipya cha wachekeshaji.

Wachekeshaji Mtumishi na Mchungaji waliwakilisha Churchill kabla ya mchekeshaji Dem wa FB na Terrence Creative anayefahamika Zaidi kwa igizo lake kama mwanamume Mkongo mwenye utajiri wa fedha za ulaghai – Papa Freddy Ngamwaya – kumaliza udhia.

View Comments