In Summary

• Wema ametamka kumkubali mia kwa mia mtoto huyo ikiwa ni baada ya kukiri kwamba amekuwa akitaabika na wazo la kupata mtoto wa kwake mwenyewe.

Wema Sepetu akiwa na mtoto wa Whozu na ex wake Tunda.
Image: Instagram

Muigizaji Wema Sepetu hatimaye amefanya uamuzi wak umchukua kabisa mtoto wa mpenzi wake, Whozu na kumkubali kama wake, baada ya majaribio kadhaa ya kupata wake kugonga mwamba.

Wema ambaye amekuwa akiishi na Whozu tangu mwaka jana, miezi michache baada ya msanii huyo wa ‘Ameyatimba’ kuachana na mama bintiye, Tunda amekuwa akionesha mapenzi kwa kinda huyo kama mama wa kumzaa.

Katika hatua nyingine kabisa, Wema Sepetu aliapakia video ya mtoto huyo akicheza na kusema kwamba kwa sasa hadi kwenda mbele huyo ndiye mwanawe wa kudumu haijalishi chochote kitakachotokea.

Napenda tu kutamka, huyu ni Mshweet wangu mimi no matter what... "My own true baby I never had..🥺" Always & Forever... Lola wa mama Mama Chimama,” Wema Sepetu alisema.

Wema ametamka kumkubali mia kwa mia mtoto huyo ikiwa ni baada ya kukiri kwamba amekuwa akitaabika na wazo la kupata mtoto wa kwake mwenyewe.

Wema katika mahojiano na Haji Manara mapema mwaka huu, alikiri kwamba amekuwa akitafuta suluhu kila kona ikiwemo kutafuta tiba asili kwa ajili ya kusafisha tumbo lake ili kupata mimba lakini juhudi zote zimekuwa bure.

 

Mapema mwaka huu alipokuwa akisherehekewa siku yake ya kuzaliwa, Wema alisimama upande wa mama na kukaa na mtoto huyo jambo ambalo liiwavutia watu mitandaoni pakubwa.

View Comments