In Summary

• "Kwa sababu hiyo, mnaponiona na yeye hakuna kitu chochote eti ooh wamerudiana, sisi ni marafiki na wazazi tu basi,” Zari alibainisha.

Zari aonekana na Diamond wiki chache baada ya kumtupia maneno ya nguoni.
Image: Instagram

Mfanyibiashara wa Uganda, Zari Hassan amekanusha uvumi wowote unaoendeshwa mitandaoni kuhusu uwezekano wake wa kurudiana na babydaddy wake, Diamond Platnumz.

Akizungumza katika uwanja wa JKIA Nairobi baada ya kutua Kenya, Zari alisema kwamba kuonekana kwake pamoja na Diamond hakuwezi kuvuka mipaka Zaidi ya malezi ya watoto wao wawili – Tiffah na Nillan – pekee.

“Diamond atasalia kuwa baba kwa wanangu, hilo halina mjadala, ni rafiki yangu, sisi sio wale maEx wanaochukiana. Sisi huongea, ni mtu ambaye ninaweza kumpigia simu kama kuna kitu kinanisibu, na yeye vile vile, kwa hiyo hakuna damu mbaya baina yetu. Kwa sababu hiyo, mnaponiona na yeye hakuna kitu chochote eti ooh wamerudiana, sisi ni marafiki na wazazi tu basi,” Zari alibainisha.

Zari ametua nchini Kenya kuhudhuria mkutano wa wanawake katika biashara – Women in Business jijini Nairobi.

Akizungumzia kuhusu kumwalika Tanasha Donna katika tamasha lake la Zari All White Party, mjasiriamali huyo alisema kwamba wao licha ya kwamba wanashiriki baba mmoja kwa watoto wao, lakini bado huwa wanazungumza na kupigiana simu.

“Zari ni rafiki yangu, huwa tunazungumza, tunapigiana simu kwa sababu kila mmoja ana maono mema kwa watoto wetu, nilikuwa na shoo na nikamwambia kama atakuja na akakubali,” alisema.

View Comments