In Summary

• Msanii Bahati na mkewe Diana Marua ni miongoni mwa watu maarufu walioalikwa na kuhudhuria.

Bahati na Diana Marua.
Image: Instagram

Mapema wiki iliyopita, mchekeshaji na muigizaji Terence Creative alikuwa na tukio lake kubwa la kuzindua filamu yake ya mwendelezo ya Wash Wash msimu wa nne.

 Katika uzinduzi huo uliofanyika usiku wa kuamkia sikukuu ya Jamhuri, mastaa mbali mbali walioalikwa na wasioalikwa walijitokeza kwa wingi kumpa shavu mwenzao katika tasnia ya ubunifu na uigizaji ya Kenya.

Msanii Bahati na mkewe Diana Marua ni miongoni mwa watu maarufu walioalikwa na kuhudhuria.

Katika uzinduzi huo, mastaa walifurika kila mmoja akiwa kwenye fasheni yake nzuri na kuchora taswira kama ya mashindano ya fasheni.

Bahati na mkewe walitokea kwenye fasheni ya kipekee ambayop ilivutia wengi katika mitandao ya kijamii na sasa wapenzi hao wakwasi wamefichua kiasi cha pesa ambazo walitumia kufanikisha muonekano wao mzuri.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Bahati alipakia picha wakiwa na mkewe katika uzinduzi wa Wash Wash 4 na kufichua kwamba iliwagharimu robo tatu za milioni kufanikisha muonekano wao mzuri, akisema kwamba hicho ni kiasi kidogo sana cha pesa kwao.

“Tulitumia 750,000 ksh kwenye mavazi yetu ya #WashWash4 🔥🔥🔥 Ilitufaa Kutumia Pesa kwa Mitindo inayofikiri nje ya Boksi,” Bahati alisema kwa kujitapa.

Hata hiyo, mkewe ambaye ni muongeaji sana alimkosoa Bahati kwa kudanganya akisema kwamba kiasi walichotumia katika mavazi yao kilizidi laki nane.

“Mpenzi wangu, ilikuwa ni 826,000. Hebu fanya hesabu yako vizuri,” Diana Marua alimkumbusha.

Baba mwenye shughuli, Terence Creative naye hakuachwa nyuma, alifika kwenye chapisho hilo na kutooa maoni yake akisema kwamba katika hiyo hesabu ya mavazi ya Bahati na Diana, ukiongeza hesabu ya mavazi yake na mkewe Milly Chebby bila shaka jumla ya hesabu inavuka Zaidi ya shilingi milioni 2 za Kenya.

View Comments