In Summary

• Alisema kwamba hivi karibuni anakwenda kumalizia muonekano wake na kuwa wa kike kabisa kwa kupata maziwa makubwa.

Kinuthia
Image: Facebook

TikToker maarufu kwa kuvaa mavazi kinyume na jinsia yake, Kinuthia amewashangaza mashabiki wake baada ya kudokeza kwamba hivi karibuni atapata maziwa makubwa na kuanza kuvaa sidiria.

Kunuthia alifichua haya katika klipu kwenye Insstory yake ambapo alikuwa anajibu maswali ya mashabiki wake ambao mara kwa mara wanamuuliza mbona anavaa mavazi ya kike pasi na kuwa na maziwa.

TikToker huyo ambaye ana umbo na muonekano wa mwanamke katika asilimia kubwa ya mwili wake, alisema kwamba hivi karibuni anakwenda kumalizia muonekano wake na kuwa wa kike kabisa kwa kupata maziwa makubwa.

“Hamjambo mashabiki zangu, natumai nyinyi wote mko salama, kwa hiyo watu wengi wamekuwa wakiniambia ooh Kinuthia unavalia rinda, ooh Kinuthia unatesa na nywele laini lakini hauna maziwa… rafiki zangu, na mnajua nini sasa nimeshapata tiba ya kuongeza maziwa…” Kinuthia alisema alitangaza chapa moja yenye kuuza bidhaa za kuongeza maziwa.

Alisema kwamba hivi karibuni atakuwa anatimba kwenye maduka ya kuuza mavazi ya kike kuangalia sidiria yenye kumtoshea na hajui watu watamsema kivipi.

“Na wacha niwaambie, hii sasa zijui zikimea nianze kuenda kujua size ni gani sijui mtakuwa mkiambia watu nini jamani juu sasa mimi ni ule wakati wa kufanya hivyo,” alisema.

Kinuthia amekuwa akipuuza maneno ya kuapiza kutoka kwa watu na kuendelea kufanya kile anachokipenda kutafuta riziki kwa kuvaa kama mwanamke.

Akianzia, watu wengi walikuwa wanamuuliza familia yake inamchukulia vipi lakini aliwashanagza wengi alipokiri kwamba mama yake ndiye shabiki wake nambari moja ambaye anampa mshawasha wa kuendelea kuvalia mavazi ya kike mradi apate riziki yake ya kila siku,

Kinuthia aliwahi sema kwamba akianza alikuwa anaomba mavazi ya mamake ili kurekodi nayo video na kupakia kwenye mitandao ya kijamii haid kujizolea umaarufu mkubwa.

View Comments