In Summary

• Ntazola safari hii amerudi na kusisima vita dhidi ya miziki ya Gengetone akisema kwamba hata kwa mtutu wa bunduki hawezi jipata anasikiliza miziki hiyo.

• Alisema kwamba kumtaka asikilize gengetone ni sawasawa na kumlazimisha kula nyama ya nguruwe.

Gloria Ntazola.
Image: Instagram

Gloria Ntazola, mrembo na mjasiriamali wa vipodozi aliyepata umaarufu wa ghafla mwaka jana baada ya kupapurana na askari wa kaunti ya Nairobi – Kanjo, amerudi tena mwaka huu kwa vishindo vya aina yake.

Ntazola safari hii amerudi na kusisima vita dhidi ya miziki ya Gengetone akisema kwamba hata kwa mtutu wa bunduki hawezi jipata anasikiliza miziki hiyo.

Mrenbo huyo akitoa sababu yake kwa uamuzi huo, alisema kwamba kwanza miziki ya gengetone haina ujumbe maana ya kusikilizwa Zaidi ya kelele tu za ala za muziki na pili urembo wake ni wa kupindukia ambao hauwezi kumpa nafasi ya kusikiliza miziki kama hiyo.

“Huwa sisikilizi miziki ya Kenya kwa sababu hakuna cha mno cha kusikilizwa mle. Na huu urembo wangu eti nijipate nasikiliza gengetone? Jamani hapana! Wasanii wenyewe ni wazembe ambao hawana hata uwezo wa kuwekeza katika Sanaa yao, heri tu tujikite katika riadha,” Ntazola alisema.

 Lakini pia, Ntazola alisema kwamba ukimtaka kufanya chaguo kati ya gengetone na miziki ya kutoka Magharibi mwa Kenya, yeye atachagua miziki ya Kiluhya pasi na kupepesa jicho.

Alisema kwamba kumtaka asikilize gengetone ni sawasawa na kumlazimisha kula nyama ya nguruwe, kitu ambacho anakichukia mno.

“Heri nisikilize nyimbo za Waluhya kuliko nikae nikisikiliza Gengetone. Kuniambia nisikilize genetone ni sawa na kunishrutisha nikule nyama ya nguruwe, kusema ukweli sipendi huyo mnyama hata kidogo,” Ntazola aling’aka.

 

View Comments