In Summary

• Kufuatia tukio hilo, Pozee alisema kwamba kuanzia sasa hivi mpaka mbeleni, yeye atasalia kuwa bila mpenzi.

Willy Paul
Image: Facebook

Msanii wa kizazi kipya Willy Paul ameanza mwaka na pigo takatifu baada ya kutendwa kimapenzi.

Msanii huyo kupitia Instagram yake alichapisha picha yake na kuiambatanisha na ujumbe wa kuonekana kutamaushwa kabisa na mapenzi.

Pozee, kama anavyojiita alisema kwamab kuanzia leo hadi mwisho wa Dahari, haoni kama ataweza tena kuamini kauli kuwa kuna mapenzi ya kweli.

Mkali huyo wa ‘Toto’ alisema kwamba sasa ndio anaamini kwamba mapenzi ni utapeli, akidokeza kwamba tayari ameshatendwa na mrembo ambaye alikuwa anamuaminia kuwa anaonesha mapenzi ya kweli kwake.

Kufuatia tukio hilo, Pozee alisema kwamba kuanzia sasa hivi mpaka mbeleni, yeye atasalia kuwa bila mpenzi lakini atazidi tu kujumuika na warembo ‘ovyo ovyo’ bila kujali kama atatulia na mmoja maishani.

“Mapenzi Yote Ni utapeli marafiki zangu. Tafadhali Usifanye! Ngoja Nikuambie Maina, Huyo mrembo Kweli kanitenda 🤣. Kuanzia Leo Niko Single Na nitazidi Kuchanganya Ovyo Ovyo,” Willy Pozee alisema.

Licha ya kuwa na ufanisi mkubwa kimuziki na kimaisha pia, Pozee ni mmoja wa wasanii ambao hajawahi kuonekana kuwa na mwanamke hadharani ambaye anasema kuwa ndiye wa maisha yake.

Maisha yake ya kimapenzi yamekuwa na hadithi changamano, kwa wakati mmoja akituhumiwa na Diana Marua kwa ubakaji, suala ambalo liliishia mahakamani na hata kusisima uhasama baina yao hata Zaidi mpaka sasa.

Uhasama wa Willy Paul na Bahati umeendelea mpaka hivi majuzi Bahati na mkewe walilazimika kujitoa katika hafla ambayo walifaa kuhudhuria huko Mwea, Jamii Gardens baada ya kubaini kwamba Willy Paul pia alikuwa ameratibiwa kuwepo.

View Comments