In Summary

• Juzi pia dirisha la ndege ya Alaska liling’oka ndege hiyo ikiwa angani, lakini ndege hiyo iliweza kutua salama salimini.

Baba Levo
Image: Instagram,

Mbwatukaji wa mitandaoni ambaye ni msiri mkubwa wa msanii Diamond Platnumz, Baba Levo ameanza mwaka 2024 akiwa na nyota ya unabii wa kuweza kutabiri matukio yajayo.

Kupitia ukurasa wake Instagram, Baba Levo amewatia woga wasafiri wengi wa ndege baada ya kudai kwamba amekuwa akiota kuhusu ajali mbaya ya ndege ambayo itatokea katika ukanda wa Afrika Mashariki mwaka huu.

Levo kwa ukakamavu alisema kwamba ndoto hiyo imekuwa ikimjia mara kwa mara tangu mwaka huu ulipoanza na ameona ni ni vyema aweze kuisema mapema ili wanaoweza kuikemea wafanye hivyo kabla majanga makubwa hajayatokea.

Hata hivyo, chawa huyo wa WCB Wasafi hakuweza kubaini ndoto hizo zake zimekuwa zikimuelekeza ajali itatokea katika nchi ipi, lakini alisema kwa ujumla ni Afrika Mashariki.

"Kila siku naota ajali ya ndege East Africa, natabiri mwaka huu 2024 itatokea ajali ya ndege ukanda wa Afrika Mashariki," Baba Levo alisema.

Ungamo hili linakuja siku chache tu baada ya matukio yanayohusisha ajali za ndege kuripotiwa katika maeneo mbalimbali ulimwenguni, ikiwa ni wiki moja tangu dunia ilikunjue jamvi la 2-24.

Itakumbukwa siku nne zilizopita, dunia ilipokea taarifa za kuogopesha kutoka Japan baada ya ndege iliyokuwa imebeba abiria 379 kutua kwa ghafla ikiwa inawaka moto.

Hata hivyo, vyanzo vya habari viliripoti kuwa Abiria na wafanyakazi wote 379 walinusurika bila kujeruhiwa baada ya ndege ya Japan Airlines 516 kuwaka moto kufuatia ajali iliyotokea.

Juzi pia dirisha la ndege ya Alaska liling’oka ndege hiyo ikiwa angani, lakini ndege hiyo iliweza kutua salama salimini.

View Comments