In Summary

· Vishy alisikika akimbembeleza Stevo kukubali japo salamu kwa njia ya kumbato lakini msanii huyo wa ‘Tuheshimu ndoa’ alibakia kwenye msimamo wake wa kutotaka mazoea na Ex wake.

Jalang'oo alimpigia simu Stevo kukataa kusalimia Vishy
Image: facebook

Mheshimiwa Jalang’oo wa jimbo la Lang’ata amefichua kuwa yeye ni shabiki wa muda wote wa rapa Stevo Simple Boy na anafuatilia kwa ukaribu mkubwa masuala yote ambayo yanaendelea kumhusu msanii huyo.

Jalang’oo alifichua ukweli huu alipokuwa akifanyiwa mahojiano na waandishi wa habari za mitanaoni katika hafla ya uzinduzi wa kolabo ya KRG na Konshens kutoka Jamaika.

Mbunge huyo alifichua kwamba hata hivi majuzi baada ya video kuvujishwa ikimuonesha msanii huyo akidinda kumpa salama aliyekuwa mpenzi wake, Pritty Vishy alimpigia simu kumpa ushauri.

“Nimekuwa shabiki wa Stevo kutoka zile enzi za ‘vijana tuache mihadarati’ mpaka walipoanza kuchumbiana na Pritty Vishy na kisha kuachana na mpaka hivi juzi nilipoona video akikataa kumsalimia Vishy. Nilimpigia simu Stevo,” Jalang’o alifichua.

Alisema katika maongezi yao kwa njia ya simu, alimshauri kuwa asiwe na roho nyeusi dhidi ya Ex wake kwani kwa kipindi Fulani ndiye alikuwa mtu wa kumpa furaha katika maisha yake na hivyo alikosea kukataa salamu tu.

“Nilimwambia huyo ni Ex wako, huyo ni mtu wako na kidogo tu mngepata mtoto. Tuliongea na yeye kwa muda mrefu nikamuambia Ex wako ni lazima umpende. Make pamoja,” Jalang’oo alisema.

Katika video hiyo ambayo ilienezwa mitandaoni, Stevo aliongozana na vijana wengine wawili na kumkuta Pritty Vishy ndani ya nyumba moja iliyokaa kama makaazi yake.

Waliketi kwa kochi lakini tevo muda wote akawa amenuna licha ya bembeleza za kina kutoka kwa Vishy akimnyooshea mkono kwa ajili ya salamu.

Vishy alisikika akimbembeleza Stevo kukubali japo salamu kwa njia ya kumbato lakini msanii huyo wa ‘Tuheshimu ndoa’ alibakia kwenye msimamo wake wa kutotaka mazoea na Ex wake.

View Comments