In Summary

• DeSagu amekuwa akivutwa kwenye mitandao ya kijamii baada ya watu kudai kwamba anamfanana na mshukiwa mkuu wa mauaji ya dadake mchungaji Kanyari, Starlet Wahu.

DeSagu na Fisi.
Image: Facebook

Mchekeshaji Henry DeSagu ameamua kutumia fursa ya ujumbe wa idara ya wanyamapori, KWS kuhusu jinsi ya kuepuka kushambuliwa na fisi, ujumbe ambao ulipokelewa kwa utani na ucheshi na Wakenya.

Baada ya Wakenya wengi kuzua utani kuhusu takwa moja la KWS kuwataka watu kutotoroka pindi wanapokutana na fisi na badala yake kusimama imara na kuzungumza nao, Desagu alipakia picha kwenye kurasa zake mitanaoni akidai kuwa amekuwa mtu wa kwanza kutii takwa hilo.

Akirejelea eneo la Juja ambako mahsambulizi ya fisi dhidi ya binadamu yameripotiwa kwa wingi, mchekeshaji huyo kutoka Mwihoko alisema kwamba alilazimika ‘kufanya mazungumzo na fisi wa Juja’ ili kutafuta mwafaka.

Kwa utani aliwaita fisi hao kwa majina ya watu.

“Mapema leo tulifanya mazungumzo na brayo & Onyi kwenye kuhusu suala la mashambulizi Juja ...ni bash zimekua nyingi hayo maeneo,” DeSagu alitania.

Wakenya ambao hawaishiwi na utani na vichekesho walifika kwenye chapisho hilo na kutoa aoni mbali mbali, wengine wakidai kuwa fisi hao wameitawala Juja kama wafalme na hivyo ni wafalme wa Juja.

Haya hapa ni baadhi ya maoni ya mashabiki wa DeSagu;

“Mfalme wa Mwihoko amekutana na wafalme wa Juja,” Njange Maina.

“Lugha gani mlikubali tuitumie kwenda mbele!” Kelvin Kimutai.

“Je, ni ajenda gani kuu iliyojadiliwa katika mkutano huo” Feddy Jeshii.

DeSagu amekuwa akivutwa kwenye mitandao ya kijamii baada ya watu kudai kwamba anamfanana na mshukiwa mkuu wa mauaji ya dadake mchungaji Kanyari, Starlet Wahu.

Jumatano, DeSagu alifutilia mbali madai hayo akisema kwamba hana uhusiano wowote na John Matara.

View Comments