In Summary

• Hata hivyo, meneja wake aliomba pesa kutoka kwa bosi wake alipojibu chapisho hilo, "Ah shiriki nazi hizo pesa ili kama ni kuchoka tuchoke pamoja basi".

• Baadaye, Davido alijibu, "Inshangaza….unanishinda, una nyingi kushinda mimi", akimaanisha kuwa Asa Asika ni tajiri kuliko yeye.

Davido na meneja wake.
Image: X

Mwimbaji maarufu wa Nigeria na bosi wa lebo ya muziki ya DMW, Davido amefichua kuwa meneja na rafiki yake, Asa Asika ni tajiri zaidi yake.

Davido aliyafahamisha hayo kupitia ukurasa wake wa X baada ya Asa Asika kumuomba pesa kwa mbwembwe kwenye mtandao huo wa blogu ndogo ndogo.

Inafaa kukumbuka kuwa baba huyo wa mapacha alisema kuwa kuwa na pesa ni kuchosha wakati una kila kitu peke yako, akisema kuwa pesa inakusudiwa kugawanywa na kutumiwa na watu wanaokuzunguka.

Aliandika, "inachosha kuwa na pesa peke yako".

Hata hivyo, meneja wake aliomba pesa kutoka kwa bosi wake alipojibu chapisho hilo, "Ah shiriki nazi hizo pesa ili kama ni kuchoka tuchoke pamoja basi".

Baadaye, Davido alijibu, "Inshangaza….unanishinda, una nyingi kushinda mimi", akimaanisha kuwa Asa Asika ni tajiri kuliko yeye.

Chapisho hilo ambalo lilionekana kuwa na utani lilivutia maoni ya watu wengi, baadhi wakimuomba Davido kuwagawia japo kiasi kidogo cha pesa hizo ambazo anadai zinamchosha akiwa nazo.

“Mtu yeyote atakayejidai kuwa na pesa kukushinda basi anafaa kuwa na nchi yake mwenyewe maana wewe umeshindikana, unatumia dola mia moja kila siku kununua kopo la msalani tu,” Prince Charmin alimwambia.

“Tufanye basi sisi tumalize kesi hii, wale ambao hatuna kitu chochote, niko tayari kuchoshwa na pesa Davido,” Ify Hill alisema.

“Mungu wangu, angalia jinsi watu matajiri wanavyofanya mzaha, mimi natamani nifikie kiwango chao japo siku moja,” mwingine aliandika.

Angalia maoni Zaidi kweney chapisho hili la X;

View Comments