In Summary

• "Kunaye mmoja wenu ambaye anajua kanisa zuri ambalo sitoweza kusumbuliwa na kuangaliwa, tafadhali pendekeza moja,” Vera Sidika aliomba.

 

Vera Sidika.
Image: Facebook

Mwanasosholaiti Vera Sidika amedai kwamba mwaka huu wa 2024 anataka kuboresha hata Zaidi uhusiano wake na Mungu.

Sidika kupitia instastory zake, alisema kwamba angependa kuanza kuhudhuria ibada kanisani katika kipindi cha mwaka huu, akisema kwamba hiyo ndio njia pekee ya kuimarisha Zaidi uhusiano wake na Muumba wake.

Kwa namna hiyo, Sidika aliwaomba mashabiki wake katika mtandao huo kumpa ushauri wa ni kanisa lipi zuri la kufanya mahudhurio ya ibada, akisema kwamba licha ya kuwa na uhusiano mzuri na Mungu, kwa muda mrefu sasa hajawai tia guu lake katika malango ya kanisa.

Mama huyo wa watoto wawili alisema kwamba aliwahi jaribu kufanya hivyo kwa wakati mmoja lakini akapata kila mtu macho yanamtoka pima pindi tu wanapomuona kanisani, jambo lililomchochea kujivuta nyuma katika suala zima la kwenda kanisani.

“Mwaka huu wa 2024 ninataka kujenga uhusiano mwema na Mungu, sijawahi kuenda kanisani kwa muda sasa, mimi ni muumini, namuomba Mungu na kufanya upande wangu kama Mkristo. Lakini inniwia vigumu kwenda kanisani. Watu wananiangalia sana. Kunaye mmoja wenu ambaye anajua kanisa zuri ambalo sitoweza kusumbuliwa na kuangaliwa, tafadhali pendekeza moja,” Vera Sidika aliomba.

Lakini pia alisisitiza kwamba asingependa kupendekezewa kanisa katika sehemu yoyote ile akisisitiza kwamba angependa kuhudhuria kanisa katika maeneo ya Kifahari ya Karen.

“Ikiwezekana iwe Karen,” Sidika aliongeza.

View Comments