In Summary

• “Nasukumwa sana kuwa mchungaji🤭 mtaniamini? mtatoa sadaka kwa uaminifu?,” Tunda aliandika Instagram.

Tunda
Image: Instagram

Miaka michache baada ya kusambaratika kwa penzi lake na babydaddy wake Whozu, mrembo Tunda amefichua kwamba amekuwa akijipata chini ya shinikizo la kitu Fulani kikiiambia nafsi yake kuwa ni muda sasa abadili taaluma yake.

Tunda, kupitia Instagram yake, alichapisha ujumbe huo akisema kwamba kwa muda sasa amekuwa akipata msukumo wa kutaka kuwa mchungaji na kuanza kulihubiri neno.

Mtoto huyo wa askari jeshi mstaafu aliyejijengea kaburi alisema kwamba japo ana msukumo wa kuanzisha kanisa lake, swali moja ambalo linamtatiza ni iwapo mashabiki wake watamuamini kuwa amebadilika na kumrudia Mungu.

Alihoji iwapo watamuamini na kama watakuwa radhi kutoa sadaka kwa uaminifu kabla ya kujitoma mazima kaitka kuifanikisha ndoto yake.

Nasukumwa sana kuwa mchungaji🤭 mtaniamini? mtatoa sadaka kwa uaminifu?,” Tunda aliandika Instagram.

Mashabiki wake wengi walionekana kumuunga mkono lakini wengine wakamwambia kuwa hiyo ni ndoto ya majaribu wakitilia shaka tamko lake kuanzia sadaka badala ya uponyaji.

Haya hapa ni baadhi ya maoni ya matumizi wa Instagram;

“Naomba niwe muweka hazina wako,” Sabrah Eagle.

“Amka utakojoa kitandani mdogo wangu kumekucha huo ni mtego,” Grace Sara Kikyaa.

“Mbona umeanza na Sadaka sio uponyaji,” Nassoro Cholo.

“Utapendeza Sana Kumtumikia Mwenyezi Mungu Anza Sasa Utaniaambia,” Dackmanb

“Sadaka labda tutoe online maana we mwenyew hutaenda kanisan mchungaj😂😂😂😂” Officila Feylee.

Mama Lola waliachana na Whozu lakini wamekuwa wakishirikiana kumlea mtoto huyo ambaye alitimiza umri wa mwaka mmoja mwaka jana.

Whozu mara kwa mara amekuwa akionekana na mwanawe wakiwa na mpenzi wake, Wema Sepetu ambaye alikiri kwamba ameamua kumchukulia mtoto huyo kama wake wa kumzaa.

View Comments