In Summary

• Mungai Eve kupitia insta stories zake, alisema kwamba bado anaendelea kujifunza mambo mengi tu kutokana na kile ambacho kimempata wiki jana.

Mungai Eve
Image: Instagram

YouTuber Mungai Eve kwa mara ya kwanza amevunja kimya na kuonekana kuzungumzia zogo linalozunguka uhusiano wake na Director Trevor pamoja na suala zima la kubadilishwa kwa majina ya kurasa za Chaneli na Facebook.

Wakati Trevor anaweka wazi kuwa huduma za Mungai Eve kama sura ya chaneli yao ya YouTube yenye wafuasi Zaidi ya laki 7, Mungai Eve alikuwa safarini kwenda Zanzibar kujivinjari.

Trevor aliweka wazi kwamba yeye na Mungai Eve si mtu na mpenzi wake tena na kwamba Eve hatoendelea kuchangia katika kukuza maudhui kwa ajili ya akaunti zao, aitangaza pia kubadilisha majina kwenye Facebook na YouTube.

Mungai Eve kupitia insta stories zake, alisema kwamba bado anaendelea kujifunza mambo mengi tu kutokana na kile ambacho kimempata wiki jana.

Hata hivyo, Eve aliashiria kwamba vitu vingine vinakaa vizuri wakati vinapuuzwa kuzungumziwa, akiahidi kwamba ataendelea kufunga mdomo wake kwani hiyo ndio tiba pekee na kuondokana na hili.

“Vibaya jinsi utakavyotaka kuvielezea, vitu vingine vinasalia vizuri vikiwa havizungumziwi. Bado naendelea kujifunza. Wakati mwingine nafasi binafsi unayohitaji ni kufunga mdomo wako, kusonga mbele na kuishi maisha yako bora,” Eve Mungai alidokeza.

Licha ya kubadilishwa kwa chaneli yao ya YouTube kutoka Mungai Eve kwenda kwa Kenya Online Media, bado baadhi ya watu wanahisi wawili hao ni wapenzi na wanajaribu kuvutia usikivu wa mashabiki wao ili kuleta mwamko mpya.

Hata hivyo, baadhi ya wengine wamemshauri Mungai Eve kwenda mahakamani ili kupata sehemu ya hisa za chaneli hiyo ambayo sasa inatawaliwa na aliyekuwa mpenzi wake Trevor.

Lakini pia wengine wamemshauri kuanzisha chaneli mpya wakimuahidi kumpa sapoti ya kipekee na kujiendeleza kama chapa huru bila muingiliano wa mtu yeyote.

View Comments