In Summary

• Stevo alisema kwamba Betty Kyallo alipomuona kwenye muonekano wake wa kibabe kwa mara ya kwanza, alishtuka na kubabaika.

Kyallo na Stevo
Image: Facebook

Stevo Simple amefichua kwamba alitumia Zaidi ya laki moja na elfu 60 kwenye muonekano wake katika mtoko na mwanahabari Betty Kyallo.

Msanii huyo alikuwa anazungumza kwa mara ya kwanza kwenye mahojiano na mwanablogu Trudy Kitui ambapo alisema kwamba viatu pekee vilimgharimu elfu 40 pesa za Kenya.

 Kwa hesabu ya haraka haraka, Stevo alifichua kwamba nguo pekee zilichukua elfu 125, na kusema kwamba alitumia kiasi hicho chote cha pesa kutokana na mapenzi yake ya dhati kwa Kyallo.

“Mavazi yangu yalinigharimu pesa nyingi. Kwanza koti, suruali na tai vyote vilichukua 125,000. Viatu peke yake vilichukua 40,000. Kwa hiyo hesabu yote ilikuja kama 165,000,” Stevo alidadavua hisabati.

Stevo alisema kwamba Betty Kyallo alipomuona kwenye muonekano wake wa kibabe kwa mara ya kwanza, alishtuka na kubabaika.

“Betty kwamba alibabaika, aliniambia eeh Stevo kwani ulikuwa umenisubiria na haya mavazi yote. Nilivaa kwa ajili yake,” aliongeza.

 Lakini pia, msanii huyo alifunguka kwa undani sababu yake kuu kumpeleka Betty Kyallo kwenye dinner.

Alisema;

“Betty Kyallo nilikuwa nataka kumuonesha upendo wangu kwake. Ilikuwa ni mwanzo tu wa mapenzi yangu na tukiendelea basi atapata mapenzi ya dhati kutoka kwangu.”

“Tulipanga kwanza kukutana na familia zetu, kutoka hapo tupange harusi lakini aliniambia nimpe muda kidogo na atanipa jibu. Betty alinifurahisha kwa kuongea, ako tu sawa. Yeye ni mcheshi na mimi ni mcheshi kwa hiyo tuliendana.”

“Gharama zote za Betty ni mimi niligharamia. Na ikitokea amenikubalia, nitampa mapenzi ya dhati, nitamuelewa naye pia anielewe, tufanye kazi pamoja, tushirikiane. Mambo yake ni yangu na yangu yatakuwa yake,” alimaliza.

View Comments