In Summary

• Msanii huyo alisema kwamba kitu ambacho kilibadilika katika uhusiano wake na Mungu ni kuacha kuimba tu injili, lakini katika misingi ya Kikristo bado yuko imara.

Willy Paul amekiri kwamba hajakuwa akienda kanisa tangu 2017.
Image: HISANI

Willy Paul, aliyekuwa msanii wa injili kabla ya kuvuka na kuingia katika miziki ya kidunia ya kizazi kipya amefunguka  uhusiano wake na Mungu tangu kuvuka mpaka.

Akizungumza baada ya kutumbuiza kwenye Boom Fest wikendi iliyopita, Willy Paul alisema kwamba yeye bado amesalia katika misingi mikuu ya Kikristo japo aliacha kuimba injili.

Msanii huyo alifichua kwamba bado yeye huomba kabla ya kuingia jukwaani kutumbuiza, sawia na alivyokuwa akifanya zamani akiwa mwinjilisti.

Msanii huyo alisema kwamba kitu ambacho kilibadilika katika uhusiano wake na Mungu ni kuacha kuimba tu injili, lakini katika misingi ya Kikristo bado yuko imara.

“Kabla nipande steji, sisi huomba hata hapa tumeomba. Kitu pekee ambacho kilibadilika kuhusu Willy Paul na Mungu ama na hii kitu watu wanaita huduma ni aina ya muziki ambayo ninafanya, lakini uhusiano wangu na Mungu bado uko imara, mimi ndio najua jinsi ninaongea na yeye,” alisema.

Akitoa kidokezo kuhusu maisha yake ya kimapenzi, Willy Paul alisema, “Wanawake, eeh! Mimi kwa kweli nawapenda sana, lakini pia nawaogopa sana!”

Msanii huyo ambaye katika siku za hivi karibuni amekuwa akipigwa vita sana mitandaoni alisema kwamba ngao yake ni kuwapuuza wote wanaozungumza vibaya na kumshushia kashfa huku pia akijua kwamba anaisha maisha yake ya uhalisia.

View Comments