In Summary

• Kuhusu msanii mwenza Ommy Dimpoz kudaiwa kuwa chanzo, Jux alisema kwamba hata yeye alisikia madai hayo katika mitandao ya kijamii lakini hajapata kuthibitisha hilo.

Jux na mpenzi wake Karen Bujulu
Image: INSTAGRAM// JUMA JUX

Kwa mara ya kwanza, msanii Ommy Dimpoz amethibitisha kuwa hayuko katika mahusiano ya kimapenzi na mrembo wake Karen Bujulu.

Katika mazungumzo na mtangazaji wa Wasafi, Lil Ommy, Juma Jux alithibitisha hilo na kusema kwamba yapata miezi mitatu sasa tangu kila mtu aanze kujishughulisha na hamsini za kwake.

“Ni kweli mimi na Karen [Bujulu] hatuko pamoja tena, imekuwa kwa muda sasa nadhani inaenda miezi 3 kama sio 4,” Juma Jux alithibitisha katika mahojiano hayo.

Kuhusu msanii mwenza Ommy Dimpoz kudaiwa kuwa chanzo, Jux alisema kwamba hata yeye alisikia madai hayo katika mitandao ya kijamii lakini hajapata kuthibitisha hilo.

Wiki chache zilizopita baada ya Jux na Bujulu kuonekana kufuta picha za kila mmoja kwenye kurasa zao Instagram na pia kutoonekana pamoja siku ya Wapendanao ya Februari 14, madai yaliibuliwa kwamba Ommy Dimpoz alimzunguka rafiki yake Jux kwa mpenziwe kupelekea kuachana kwao.

“Ommy Dimpoz ndiye alikuwa chanzo kama ambavyo ilisemekana, kuhusu Ommy, hicho ni kitu ambacho pia mimi nimekisikia kama ambavyo nyinyi mnavyosikia. Si kitu ambacho mimi najua au ninaweza sema sio au sicho,” Jux alisema.

Jux amekuwa si mwenye bahati katika mapenzi kwa miaka sasa tangu alipolipoteza penzi lake kwa mrembo Vanessa Mdee ambaye penzi lake liliota upya katika mtima wa msanii na muigizaji wa Marekani mwenye usuli wa Nigeria, Rotimi.

View Comments