In Summary

•“Hii ark si kama ile ya Noah. Hii iko na televisheni ndani, Wi-Fi, kitchen, Iko na bedrooms nne. Choo mbili, migahawa. Yaani ni safina ya Gen Z.” Eric alisema.

•Hiyo Ark vile Kenya inaenda na vile serikali inapanga vitu, hiyo Ark tutaitumia sana.

Eric Omondi
Image: Facebook

Mwanaharakati nchini Kenya na mcheshi Eric Omondi amefichua vipengele vya kipekee ndani ya safina yake mpya.

Akizungumza na waandishi wa habari, Eric Omondi alifichua mambo ambayo hayajulikani katika safina yake mpya aliyoijenga, akisema ni ya aina yake kwani imewekwa na sifa za kipekee ndani kwa sababu ni Gen Z ark.

“Hii ark si kama ile ya Noah. Hii iko na televisheni ndani yake, Wi-Fi, jiko, Iko na vyumba vya kulala nne,choo mbili na migahawa. Yaani ni safina ya Gen Z.” Eric alisema.

Anaendelea kusema kuwa safina tayari imekamilika na wanaenda kuizindua hivi karibuni, ila tu wamebadilisha ujumbe kwa sababu hakuna mafuriko tena, ambayo ilikuwa kusudi lake na kazi ya kuwaokoa watu.

Eric pia alitoa ufahamu kuhusu  Safina na kusema ina uwezo wa kubeba watu 250, na ana mipango mikubwa zaidi ya safina.

“Hiyo ark vile Kenya inaenda na vile serikali inapanga vitu, hiyo ark tutaitumia sana. Nataka iende kaunti zote 47. Itakua ya watu. Na bado itakua inabeba chakula, mahindi, unga na nguo.”Ericalisema.

Eric anaamini kwamba kwa kuweka magurudumu kwenye Safina, itatimiza kusudi lake linalofaa.

Ark imeisha tutaizindua hivi karibuni tumebadilisha majukumu kwa sababu mafuriko yameisha. Tunataka kuiekea miguu kama gari,” Eric said.

Eric Omondi alikuwa ametangaza awali kuwa anajenga Safina ambayo ilinuiwa kuwasaidia Wakenya wengi waliokuwa wakisombwa na mafuriko, lakini sasa mafuriko hayapo tena, anapanga kuitumia kwa njia tofauti. Kusudi halibadilika, ingawa.

View Comments